Rais wa Zimbabwe
Robert Mugabe alisisitiza jumatano kuwa bara la Afrika linaweza
kujiondoa kutoka kwa Umoja wa Mataifa iwapo mahitaji yao ya kupewa viti
vya kudumu katika baraza hilo la usalama hayatasikizwa.
Akizungumza wa
wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika ili kumpongeza kwa mafanikio yake
katika kipindi chake cha utawala kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika
mwaka wa 2015,Mugabe alisema kuwa bara la Afrika limechoka kudhoofishwa
na baraza hilo la usalama.
"Nilisema katika
hotuba yangu kama mwenyekiti anayemaliza kipindi chake cha utawala cha
Umoja wa Afrika mwezi wa Januari, kwamba wakati umefika sisi wanachama
wa bara la Afrika kuwaambia wazungu tunaweza kujiondoa na kuunda shirika
lingine,"Mugabe alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni