Serikali
ya Tanzania imesema kuwa ifikapo Juni 16, mwaka huu itavifungia vifaa
vya mawasiliano vya mkononi haswa simu na tableti ambavyo vinatumia
namba za usajili bandia, mamlaka ya mawasiliano nchini
Tanzania(TCRA)ilisema siku ya Jumatano.
Meneja
wa mawasiliano makao makuu innocent mungy, aliiambia shirika la habari
la xinhua kuwa serikali ya Tanzania tayari imezindua mfumo wa rajisi ya
namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano na inawataka watoa huduma
wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa
kumbukumbu za namba tambulishi ya vifaa hivyo (IMEI)
Serikali imetetea hatua hiyo na kusema kuwa ni moja wapo ya njia ya kudhibiti wizi wa simu na kuhimiza utii wa sheria nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni