Serikali ya
India imesema kuwa itachukua hatua didhi ya genege la watu
liliomshambulia msichana wa uraia wa Tanzania, katika mji wa Bengaluru
kusini mwa nchi.
"Tumeudhika sana
na tukio hili la kuaibisha ambalo linahusisha msichana wa Tanzania,"
Sushma Swaraj, waziri wa mambo ya nje alisema kupitia ujumbe wa Twitter.
Hapo awali ubalozi wa Tanzania nchini India ulitoa taarifa ukitaka
serikali ya India kuchukua hatua zinazofaa kuhusu kisa hicho cha
kusikitisha.
Msichana huyo
mwenye umri wa miaka 21, ambaye yuko nchini India kwa masomo,
alishambuliwa na genge la zaidi ya watu 200 alipokuwa akipita karibu na
eneo la ajali ambapo mwanamke mmoja alikuwa amegongwa na gari lingine na
kisha dereva wa gari hilo kutoroka.
Inasemekana kuwa
genge hilo lilimuelekezea hasira msichana huyo kwa kumburuza kutoka
kwenye gari alimokuwa, kisha wakamvua uchi na kuliteteketeza gari lake.
Afisa mkuu wa polisi mjini Bengaluru aliambia waandishi wa habari kuwa
polisi wanachunguza kisa hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni