Makumi ya maelfu
ya watu kutoka miji mbalimbali nchini Italia wameandamana katika mji
mkuu wa nchi hiyo, Roma kupinga mpango wa serikali wa kutaka kuhalalisha
kisheria ndoa za watu wa jinsia moja.
Waandamanaji hao
walikusanyika jana katika moja ya maeneo makuu ya kale la Circus
Maximus mjini Roma wakitaka kufutwa uamuzi wa kuujadili mpango huo wa
serikali katika bunge la nchi hiyo.

Franco Pantuso,
mwenye umri wa 71, ambaye alikuwa mmoja wa waandamanaji amesema:"Sheria
hii inapingana na Mungu na inapingana na Biblia; mimi ni babu, lazima
watoto wetu na wajukuu zetu walindwe".
Itakumbukwa kuwa
wiki iliyopita Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katoliki alitoa
angalizo kali la upinzani wa Kanisa dhidi ya ndoa za watu wa jinsia moja
aliposisitiza kuwa familia ya jadi ni "familia anayoitaka Mungu".
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni