Mahakama
moja nchini Nigeria imepinga ombi la kuachiliwa huru kwa dhamana mkuu
wa harakati ya Biafra inayopigania kujitenga na Nigeria.
Mtandao
wa habari wa Africa Time umeripoti habari hiyo na kusema kuwa, mahakama
moja nchini humo imekataa ombi la kuachiliwa huru kwa dhamana Nnamdi
Kanu, mkuu wa harakati ya kupigania kujitenga na Nigeria eneo la Biafra
la kusini mwa nchi hiyo pamoja na watuhumiwa wengine wawili
wanaokabiliwa na tuhuma za usaliti na imetoa amri ya watuhumiwa hao
kubakia korokoroni hadi kesi yao itakaposikilizwa tena tarehe 9 mwezi
huu wa Februari.
Jaji John
Tsoho wa mahakama ya fiderali ya mjini Abuja, ametoa hukumu hiyo na
kusisitiza kuwa, watuhumiwa hao hawapaswi kuachiliwa huru hata kwa
dhamana.
Jaji huyo
ameongeza kuwa, kuachiliwa huru kwa dhamana watuhumiwa hao kutaharibu
uchunguzi unaoendelea kuhusu tuhuma zinazowakabili. Pia amesema, mkuu wa
harakati ya kujitenga Biafra na Nigeria huenda akatoroka nchi na
asishiriki tena kwenye vikao vya kusikiliza kesi yake kutokana na kuwa
na uraia wa nchi mbili za Nigeria na Uingereza.
Itakumbukwa
kuwa jimbo la Biafra la kusini mwa Nigeria limeshuhudia vita vibaya
sana vya wenyewe kwa wenyewe kwa karibu nusu karne.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni