Njile
Gonga (28) Huyu ndiye Jangili anadaiwa kutungua helkopta katika pori la
Akiba la Maswa lililopo katika Wilaya ya Meatu Mkoani, ambapo katika
tukio hilo rubani wa helkopta hiyo Rodgers Gower (37) raia wa uingereza
huku Mwenzake Nicholas Beste (43) raia wa Afrika Kusini akinususrika
kifo.
Iddy Mashaka (49) ambaye ndiye alikuwa Mkuu wa kitengo cha
Interejensia katika hifadhi ya taifa Ngorongoro, ambaye anadaiwa kuwa
kiunganishi Mkuu wa kutekeleza tukio la kutunguliwa kwa helkpta hiyo.
Hali ya ulinzi na usalama ilivyokuwa imehimarsihwa mahakamani pamoja na kituo cha polisi Bariadi leo hii.
Hii
ni kama haijawahi kutokea kwa wakazi wa Mji wa Bariadi, Kwa mara ya
kwanza kufurika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya hiyo kushuhudia
watuhumiwa hao.
WATUHUMIWA wa tukio la kutungua ndege aina ya Helkopta na kumuua
rubani wake Rodgers Gower (37) raia wa uingereza lilitokea mnamo tarehe
29/01/2016 katika pori la akiba Maswa wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu, leo
(jana) wamefikishwa mahakani kusomewa mastaka yanayowakabili.
Watuhumiwa hao walifikishwa katika mahakama ya Mkoa wa Simiyu,
chini ya ulinzi wa mkali wa askari polisi, huku umati mkubwa wa wananchi
wa mji wa bariadi waifurika kushuhudia watuhumiwa hao.
Akiwasomea mashtaka watuhumiwa hao Wakili mwandamizi wa serikali
Mkoa wa Simiyu Yamiko Mlekano alisema kuwa washitakiwa wote 9
wanakabiliwa na kesi tatu ambazo ni Uhujumu uchumi, mauaji pamoja na
umiliki wa siraha bila ya kibali cha serikali zenye mashtaka tofauti.
Katika kesi ya Uhujumu uchumi iliyosomwa chini ya Hakimu mkazi
mfawidhi mwandamizi wa mahakama hiyo John Nkwabi katika shtaka la kwanza
mtuhumiwa namba moja Iddy Mashaka (49) anatuhumiwa kujihusisha na
kuratibu tukio la uhujumu uchumi kinyume na kifungu 4(1)(d) sura (57)
(1) na 60 (2) cha makosa ya uhujumu uchumi sheria namba 200 iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Mlekano alisema kuwa katika kosa hilo mshitakiwa kati ya tarehe 6
januari na 1/02/2016 katika wilaya ya Meatu Mkoani Simiyu aliwashauri
Mshitakiwa namba mbili Shija Mjika (38) kuua wanayama wasiyoruhisiwa
kama tembo.
Katika shtaka la pili wakili huyo aliwataja watuhumiwa namba mbili
hadi tisa ambao ni Shija Mjika (38) Njile Gunga (28), Dotto Pangali
(42) Moses Mandagu (48) Dotto Huya (45), Mwigulu Kanga (40) Mapolu Njige
(50) pamoja na Mange Barumu (47), watuhumiwa kwa kosa la uhujumu
uchumi.
Katika shtaka hilo wakili aliieleza mahakama kuwa kati ya tarehe
21/01/2016 na 29/01/2016 katika wilaya ya Meatu, watuhumiwa hao
walipanga na kuratibu tukio la kuwinda wanyama aina ya tembo bila ya
kibali cha serikali.
Hata hivyo wakili huyo alieleza kuwa katika shtaka la tatu
watuhumiwa namba mbili hadi tisa waliotajwa hapo mwanzo, watuhumiwa
kujihusisha na uwindaji wa wanyama wasiyoruhusiwa kinyume na kifungu
47(a)(aa) cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 sambamba na sura 14 (a) na
kifungu 57 (1) cha uhujumu uchumi sura 200 iliyofanyiwa marekebisho
2002.
Alisema katika shataka hilo mnamo kati ya tarehe 26/01/2016 na
29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba katika kijiji cha Makao wilayani
Meatu watuhumiwa walimuua tembo mwenye dhamani ya shilingi Milion
32,891,100 bila ya kibali cha serikali.
Katika shtaka la nne watuhumiwa namba mbili hadi tisa wanatuhumiwa
kwa kosa la kumiliki nyara za serikali kinyume cha sheria namba
86(1)(2)(b) cha uhuwifadhi wa wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na
sura ya 14(d) na sura 57(1) cha uhujumu uchumi sura ya 200.
Katika maelezo ya kosa hilo ilidaiwa mahakamani hapo kuwa
washtakiwa kati ya 29/01/2016 na tarehe 6/02/2016 katika wilaya ya meatu
mkoa wa simiyu walikamatwa na nyara za serikali ambazo ni meno ya tembo
yenye uzito wa kilo 31 yenye thamani Milioni 32,891,100 bila ya kibali
cha serikali.
Katika shtaka namba tano watuhumiwa namba moja na mbili ambao ni
Iddy Mashaka (49) pamoja na Shija Mjika (38) wanatuhumiwa na uuzaji wa
nyara za serikali kinyume na kifungu cha sheria 84(1) cha uhuwifadhi wa
wanyama pori sheria No 5/2009 sambamba na sura ya 14(b) na sura 57(1)
cha uhujumu uchumi sura ya 200.
Katika
kosa hilo wakili alisema kuwa kati ya tarehe 6/01/2016 na tarehe
1/02/2016 katika wilaya a Meatu Mkoani Simiyu, watuhumiwa walikamatwa
wakiwa wanajihusisha na uuzaji wa nyara za serikali bila ya kibali.
Hata hivyo katika kesi namba mbili ya Mauaji wakili Mlekano
aliiambia mahakama kuwa watuhumiwa ambao ni Shija Mjika (38), Njile
Gunga (28) Dotto Pangali ( 42) pamoja na Moses Mandago (28) wanashtakiwa
kwa kosa la mauaji kinyume che sheria ya 196 na 197 cha kanuni ya
adhabu namba 16 iliyofanyiwa mwaka 2002.
Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao mnamo tarehe
29/01/2016 katika hifadhi ya Mwiba kijiji cha Makao wilaya ya Meatu
Mkoani Simiyu walimuua rubani wa ndege aina ya helkopta rubani wake
Rodgers Gower (37) raia wa uingereza.
Katika kesi zote Mbili kwa mujibu wa hakimu huyo alisema kuwa
watuhumiwa hawatakiwi kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa
na uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, ambapo keshi hizo zilihairishwa mpaka
terehe 24/02/2016 mpaka zitakapotajwa tena.
Sambamba na hayo katika kesi ya tatu ambayo ni kukutwa na siraha
kinyume cha sheria na pasipo leseni ilisikilizwa katika mahakama hiyo
chini ya Hakimu mfawidhi wa wilaya Bariadi Mary Mrio ambapo watuhumiwa
walikabiliwa na mashitaka matano.
Watuhumiwa hao ni Mange Buluma,Shija Mjika,Dotto PanganiNjile
Ngunga,Moses Mandagu,Dotto Huya na Mwigulu Kanga ambapo baadhi yao
walikiri kumiliki siraha kinyume cha sheria pamoja na riasi akiwemo
njile aliyetungua helkopta hiyo.
Watuhumiwa hao ambao Shija Mjika, Moses Mandagu, Njile Ngunga
pamoja na Dotto Pangani walikiri mashtaka mawili ambayo ni kukutwa na
siraha aina ya bunduki Riffle 303 Namba 06490 kinyume cha sheria pamoja
na risasi mbili.
Hata hivyo Njile Ngunga pamoja na Moses Mandagu walikiri pia
katika shtaka la tatu, nne pamoja na tano la kukutwa na siraha bila ya
kibali, kumiliki risasi bila ya kibali, pamoja na kumiliki tena risasi
kinyume cha sheria huku wengine kati ya hao wakikana makosa hayo.
Hata hivyo mahakama haikuweza kutoa hukumu juu ya watuhumiwa hao
waliokiri kutokana na vielelezo kutokuwepo mahakamani hapo, ambapo kesi
hiyo ilihairishwa mpaka kesho (Leo).
Watuhumiwa wote walirudishwa rumande.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni