Na Jacquiline Mrisho- MAELEZO
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi wenye malalamiko yanayohusu huduma zitolew
azo na makampuni ya simu kutosita kupeleka malalamiko yao kwenye makampuni husika.
azo na makampuni ya simu kutosita kupeleka malalamiko yao kwenye makampuni husika.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy ameyasema hayo leo jijini
Dar es salaam katika mahojiano maalumu alipokua akijibu swali kuhusu
malalamiko ya wananchi juu ya huduma zinazotolewa na makampuni
mbalimbali ya simu hapa nchini.
Amesema mteja ana wajibu wa kujua
matumizi na gharama za huduma za mitandao anazotumia pia ana haki ya
kutoa malalamiko kwa kampuni husika ili aweze kupatiwa majibu na endapo
hatasikilizwa anaruhusiwa kuwasiliana malalamiko yake Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania
Bw. Mungy ameongeza kuwa,wananchi wanaweza kufikisha malalamiko yao TCRA kwa kupiga simu au kutuma ujumbe mfupi kwenda namba 0784558270 au barua pepe;malalamiko@tcra.go.tz na malalamiko hayo yatafanyiwa kazi haraka.
Aidha, amefafanua kwamba,TCRA
haipangi bei elekezi kwa makampuni hayo hivyo gharama za mawasiliano
ziko kwenye mifumo mbalimbali kutegemeana na gharama za uendeshaji wa
huduma kwenye kampuni husika.
“Mwananchi halazimishwi kutumia
huduma ya mtandao mmoja wa simu ana uhuru wa kuchagua na kutumia mtandao
wowote wenye unafuu kwake” Amesisitiza.
Amewaomba wananchi waelewe kwamba
soko la makampuni ya simu limekuwa na ushindani mkubwa jambo
linaloyalazimisha makampuni yanayotoa huduma kubuni ofa mbalimbali kwa
lengo la kuvutia wateja.
“ Sasa hivi soko la makampuni ya
simu limekuwa na ushindani mkubwa nchini, jambo linalofanywa na
makampuni hayo ni kuweka ofa mbalimbali ambazo hizo huwasaidia wananchi
kupunguza gharama za matumizi ya simu”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni