TANGAWIZI
ni chakula cha asili chenye uwezo wa kupambana na ugonjwa wa
kichefuchefu na kutapika. Uwezo huu hutokana na vitamin B6 iliyopo kwa
kiasi kikubwa katika tangawizi ambayo ni maarufu duniani kote kwa
matumizi kama kiungo ‘spice’ kwa vyakula vingine.
Vitamin
B6 iligunduliwa mwaka 1934 na Dr. Paul Gyorgy huko Hungary na
akabainisha wazi kuwa ml.100 za B6 ni dozi tosha kwa siku kwa wagonjwa
wenye umri wa miaka 19 hadi 70 katika kupambana na kichefuchefu na hata
kuzuia kutapika pia.
Tangawizi
licha ya kuwa na uwezo wa kumaliza tatizo hili, bado imegundulika kuwa
na uwezo tena wa kukinga maradhi ya uvimbe ndani ya mwili wa binadamu
ambao husababisha wengi kupatwa na maradhi ya saratani za aina tofauti
tokana na uvimbe huo.
Hata
hivyo, ukiwa unatumia tangawizi katika kila mlo wako kwa muda mfupi tu
utajikuta maumivu ya mgongo, kiuno, maungio ya miguu na mikono
yamepungua na kama siyo kuisha kabisa. Hii ndiyo kazi halisi ya
tangawizi duniani na leo ni fursa kwako kulijua hili.
Kichefuchefu
ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi duniani na chanzo kikiwa ni kupanda
kwa joto la mwili kunakosababishwa na homa au maambukizi ya bakteria wa
maradhi tofauti yakiwemo malaria pia. Hata hivyo, ugonjwa huu huwakumba
sana akina mama wajawazito na kujikuta wakitapika mara kwa mara na
kupoteza maji na madini mengi mwilini na kuhatarisha maisha yao wenyewe,
watoto waliomo matumboni na pengine kuhatarisha maisha yao wote mama na
mtoto.
Mbali
na akina mama wajawazito kuugua ugonjwa huu watu wengine ambao hukumbwa
na ugonjwa ni wasafiri wa baharini, wagonjwa wanaotumia dawa kali,
watumiaji wa mihadarati, walaji wa vyakula vyenye sumu baridi, walevi wa
kupindukia na pengine hata wanaokutana na harufu mbaya na kali kushinda
uwezo wa kuimudu pia hupatwa na kichefuchefu na mwisho ni kutapika.
Ukiachana
na sababu hizo, bado pia wagonjwa wa kidole tumbo yaani
‘appendix/appendiatis’ au hata wanaougua magonjwa ya mchafuko wa tumbo
kama kuharisha na kipindupindu pia hupatwa na kichefuchefu na hutapika
sana wanapokosa msaada wa tiba.
Kwa
maradhi haya, kitu cha haraka kukifanya ni kunywa maji mengi huku
ukijikongoja umwone daktari haraka kwa kuwa aina nyingi za maradhi haya
huua haraka sana kwa kukosa maji na madini muhimu mwilini kwa kutapika.
Ila, ulimwengu wa kisasa umetuletea teknolojia sahihi zinazokubalika
duniani kote kwa kutengeneza vyakula lishe ambavyo ni mkandamizo wa
vitamini, madini na tindikali muhimu kwa afya. Vyakula hivi vyenye
kanuni ya vidongelishe na ungalishe vipo vya aina nyingi tu madukani na
vinasaidia watu kupona maradhi mbalimbali bila kwenda hospitali.
Kama
hujatumia tangawizi kwa muda mrefu na unajihisi kuwa na kichefuchefu
mara kwa mara basi unaweza kuanza kutumia mara moja japo hutaona matokeo
haraka ila ukitumia dawalishe ya B6 basi utapata nafuu haraka sana.
Akina
mama wajawazito wao wanashauriwa kutumia dawalishe yao maalum iitwayo
‘Pregnancy Shake’ na MOM2B ya vidonge ambayo pamoja na vitamins nyingi
zilizomo humo pia kuna vitamin B6 ambayo itamfanya ajisikie mwenye afya
njema siku zote atakazobeba mimba yake huku akijihakikishia kujifungua
salama.
Kama
wewe huna maradhi yoyote ila ungependa kujiwekea kinga ya kutosha kwa
maradhi basi unashauriwa utumie Dawalishe za B6 au uanze mara moja
kuihusisha tangawizi katika milo yako yote ya kutwa nzima na hakika
utaonekana ukitabasamu muda wote kwa kuwa utakuwa na kinga ya maradhi,
hutaumwa viungo na hutasikia kichefuchefu tena katika maisha yako.
Ukiona
mtu anatapika, basi chemsha maji yenye tangawizi yapooze na umpe anywe
na kutapika kutaisha huku ukimuwahisha kwa daktari kwa msaada zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni