Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine
Shigela akitoa taarifa ya hali ya miundombinu katika mkoa wa Tanga kwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ofisini
kwake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda
cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa pili kulia)
akimwonesha moja ya nyaraka Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli
Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (wa pili kushoto) kabla ya kusaini
makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli
kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu kushoto) akijadiliana jambo na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw.
Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la
Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart
(kushoto) wakisaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho
kwa njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Huku
Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
wakishuhudia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akiteta jambo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja Kadogosa (kulia)
kabla ya kusaini makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa
njia ya reli kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Katikati ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw.
Reinhart Swart.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (wa tatu
kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji
cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart Swart (wa tatu kulia) pembeni ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Bw. Masanja
Kadogosa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo baada ya kusaini
makubaliano ya kusafirisha saruji ya kiwanda hicho kwa njia ya reli
kutoka Tanga kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza. Kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart
Swart na (Kushoto) ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akisaidiana na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kiwanda cha Saruji cha Tanga (Simba Cement), Bw. Reinhart
Swart (wa pili kulia) wakipakia mfuko wa saruji kwenye kontena kabla ya
kuanza kusafirishwa kwa njia ya reli kutoka katika kiwanda cha Simba
Cement kwenda mikoa ya Kigoma na Mwanza.
………………………………………………………………………………………………….
Kiwanda cha Saruji Tanga (Simba
Cement), kimeingia makubaliano na Shirika la Reli Tanzania (TRL),
kusafirisha shehena ya saruji kwa njia ya reli kutoka mkoani Tanga
kwenda mikoa ya Mwanza na Kigoma.
Chini ya Makubaliano hayo zaidi
ya tani laki nne na nusu zitasafirishwa kwa mwaka na hivyo kupunguza
gharama ya bei ya Saruji katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Magharibi
kutokana na usafirishaji wa reli kuwa wa bei nafuu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema katika mkataba huo TRL litapata
zaidi ya shilingi Bilioni 40 na hivyo kufufua huduma ya usafirishaji wa
mizigo katika reli ya kati na kuongeza mapato kwa nchi.
Prof. Mbarawa amewataka
wafanyabiashara nchini kuanza kutumia reli kusafirisha bidhaa zao, kwani
usafiri huo ni salama na nafuu na unachukua shehena kubwa kwa wakati
mmoja.
“Asilimia 95 ya mizigo hapa
nchini inasafirishwa kwa barabara hivyo mkakati wa Serikali wa kufufua
viwanda utafanikiwa kwa haraka endapo wasafirishaji watatumia njia ya
reli “, amesema Prof. Mbarawa.
Aidha, amefafanua kuwa
usafirishaji wa reli ukiimarika utapunguza ajali za barabarani
zinazosababishwa na malori na kupunguza kasi ya uharibifu wa barabara
unaotokea sasa kutokana na maroli kuzidisha uzito.
Prof. Mbarawa amewataka watumishi
wa TRL na wananchi kulinda miundombinu ya reli na kutumia fursa ya
usafiri huo kujiongezea mapato.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw.
Martine Shigela amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya reli utatoa
fursa za ajira na kuwezesha bandari ya Tanga kupata shehena kubwa ya
mizigo na hivyo kurudisha hadhi ya Mkoa wa Tanga.
“Tanga tuna reli, barabara na
bandari hivyo tukio la kuanza kusafirisha mizigo kwa njia ya reli
itaongeza shehena kubwa katika bandari ,itatengeneza ajira kwa wakazi wa
Tanga na kukuza uchumi wa mkoa”, amesema Bw. Shigela.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Reli (TRL) Bw. Masanja Kadogosa amesema kusainiwa kwa
mkataba huo kutawezesha TRL kusafirisha tani elfu thelathini na tano za
Saruji kati ya tani laki moja na elfu tano zinazozalishwa na kiwanda
hicho.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda
cha Saruji Tanga Bw. Reinhart Swart, amesema usafirishaji wa Saruji kwa
njia ya reli utaongeza kasi ya usafirishaji wa saruji na kuwezesha
kuwafikia watumiaji kwa bei nafuu.
Kiwanda cha Saruji Tanga kinakuwa
kiwanda cha kwanza kuingia mkataba na TRL kusafirisha shehena ya mizigo
tangu Serikali kuanza mikakati yake ya kufufua reli na kupunguza
usafirishaji wa shehena kubwa kwa njia ya barabara na hivyo kuzuia
uharibifu wa barabara na kupunguza ajali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni