Akizungunza na Mbeya City Fc muda mfupi baada ya kumalizika kwa mazoezi ya asubuhi kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, Kocha Phiri alisema kuwa hana tatizo na nafasi ya 10 iliyopo timu yake hivi sasa kwenye msimamo wa ligi kwa sababu anaamini ushindi kwenye michezo miwili ijayo utakifanya kikosi chake kusogea mpaka nafasi ya 8.
“Msimamo wa ligi unaonyesha tuko kwenye nafasi ya 10, hili siyo tatizo sana kwa sababu kushinda mechi mbili zijazo kutatuingiza kwenye timu nane bora, hili ndiyo lengo letu, tunayo michezo minne mbele nina uhakika kwamba kila mchezaji anafahamu kuwa tunatakiwa kuongeza pointi zaidi ili tumelize ligi tukiwa sehemu ya timu nane za juu” alisema.
Akiendelea zaidi Kocha Phiri alisema kuwa kwenye mchezo huo wa morogoro kikosini atawakosa nyota kama Raphael Daud anayeguza majereha ya mguu pia mlinzi Haruna Shamte aliyekwenye zuio la kucheza kufuatia kadi za njano, huku pia akiwakosa Haruna Moshi Boban na nahodha Temi Felix ambaye kwa muda mrefu amekuwa nje ya kikosi kutokana na matatizo ya kifamilia.
“Ni wazi hatutakuwa na Haruna Moshi Boban anayesumbuliwa na maralia, pia tunamkosa Temi, tunafahamu alikuwa nje ya timu akishughulikia masuala ya kifamilia amerudi kambini juzi hivyo kwa vyovyote hawezikuwa sehemu ya mchezo huo, Rahael Daud ni mgonjwa na Haruna Shamte ana zuio la kadi za njano, kutokuwepo kwao hakuondoi dhamira yetu ya kushinda mchezo kwa sababu tumekuwa namaandalizi mazuri na muhimu kwa wachezaji wetu wengine ambao sasa wako tayari” … alimaliza Kocha Phiri na kutaja baadhi ya nyota wakaosafiri tayari kwa kuivaa Mtibwa Sugar jumamosi hii.
Miongoni mwa nyota ambao kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Malawi aliwataja ni pamoja na Juma Kaseja, Haningtony Kalyesubhula,John Jerome, John Kabanda,Yusuph Abdalah,Deo Julius, Tumba Lui,Hassan Mwasapili,Kenny Ally, Hamidu Mohamed, na Meshack Samwel na kusema kikosi chake kinataraji kuanza safari jioni ya leo moja kwa moja kuelekea wilayani Turiani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni