Akizungumza muda mfupi baada ya kuwasili kwenye kambi ya City akitokea mkoani Geita, Mwakatundu anayecheza kwenye eneo la kiungo alisema kuwa anamshukuru mungu kurejea salama kutoka kwenye majukumu kwa timu ya Geita na sasa anafungua ukurasa mpya wa kuitumia timu yake.
“Nilijiunga na Geita Gold Sports kwa mkopo mwezi januari, Nimecheze mechi zote za za ligi Daraja la kwanza na pia mechi mbili za kombe la FA, nashukuru mungu nimerudi salama sasa nawekea akili yangu kwenye timu yangu, Nawashukuru viongozi na mashabiki wa timu ya Geita kwa ushirikiano wao, hakika wamefaanya kila jema kwangu na nimejifunza mengi kutoka kwao”.
Kuhusu matokeoa ya mwisho wa michezo ya ligi daraja la kwanza kwa timu aliyokuwa akiitumikia, Mwakatundu alisema kuwa, ni viongozi wa Geita Gold pekee ndiyo wanaweza kulizungumzia hilo jambo kwa sababu yeye kama mchezaji majukumu yake yalikuwa uwanjani na anashukuru aliyatimiza asilimia 100.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni