Advertisement
Kim alipatikana na makosa ya kufanya ujasusi
Raia wa Marekani amefungwa jela miaka 10
na kazi ngumu nchini Korea Kaskazini baada ya kupatikana na makosa ya
kufanya ujasusi, shirika la habari la Uchina la Xinhua limeripoti.
Kim Dong-chul, raia wa Marekani aliyezaliwa Korea Kusini, alikamatwa mwezi Oktoba mwaka jana.
Kim aliwasilishwa kwa wanahabari mjini
Pyongyang mwezi jana na akaoneshwa akikiri makosa, na kusema kwamba
alilipwa na Korea Kusini kufanya ujasusi.
Mwezi Machi, mwanafunzi mwingine Mmarekani alifungwa jela miaka 15 kwa kujaribu kuiba bango la propaganda.
Alipatikana na makosa ya "uhalifu dhidi ya dola”.
Mhubiri wa Canada afungwa maisha Korea Kaskazini
Waziri auawa kwa kusinzia mbele ya rais
Kim amefungwa jela katika kipindi ambacho
uhusiano baina ya Korea Kaskazini na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi
nyingine za Magharibi umedorora.
Majuzi, Pyongyang imefanya msururu wa
majaribio ya kurusha makombora baada ya kufanyia majaribio bomu ya
nyuklia mwezi Januari, majaribio yote yakivunja vikwazo zilivyowekwa na
UN.
Pyongyang ilijaribu kurusha makombora
mawili ya masafa ya wastani Alhamisi lakini yalilipuka na kuanguka
baharini muda mfupi baada ya kurushwa.
Hatua hiyo ilipelekea kuitishwa kwa mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni