.

.

01 Mei 2016

MKUU WA WILAYA ATEMA CHECHE MBELE YA BARAZA LA MADIWANI

Na Sebastian Emmanuel Jr, Mafinga

Awataka wasimamie maslahi ya wananchi, waachane na ujimbo
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Mh Jowika Kasunga tarehe 29/04/2016 amehudhuria kikao cha baraza la madiwani ambapo alipata nafasi ya kuzugumza na madiwani masuala kadhaa ikiwamo lile lililokuwa likipenyeza kwenye vichwa vya wakazi wa Wilaya hiyo juu ya mgawanyiko wa madiwani ambao unaonekana kusababishwa na misimamo ya madiwani hao kuhusu ujenzi na vipaumbele vya miradi ya maendeleo ya halmashauri hiyo.
Amewaonya madiwani hao , kuwa waachane na tabia hiyo kwa kuwa haitawasaidia badala yake wataendelea kufalakana na kusahau wajibu walio nao kuwa ni kuwatetea wananchi walio waamini na wachagua. Mh Kasunga amekwenda mbali zaidi kuwa kama ikiwa hata wabunge wanamitizamo hiyo waachane mara moja wasisahau kuwa Mufindi ni moja na wananchi ni wamoja isipokuwa wanatofautiana maeneo ya kiutawala tu. Tumsikilize hapa akisema

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni