Muimbaji
mkongwe wa muziki nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ Ijumaa hii
amepelekwa Life and Hope & Rehabilitation Centre (Sober House)
iliyopo Bagamoyo kwa ajili ya kusaidiwa kuanacha na matumizi ya Madawa
ya kulevya, uongozi wa sober hiyo umethibitisha.
Hatua
hiyo imekuja ikiwa ni siku moja toka aonekane katika video iliyosambaa
katika mitandao ya kijamii ikionyesha jinsi anavyosaidiwa na jeshi la
polisi baada ya kudaiwa kutaka kijichoma kisu.
Mmoja
kati ya wasimamizi wa kituo cha Life and Hope & Rehabilitation
Centre (Sober House) ambacho pia kilimsaidia Chidi Benz kuachana na
matuzi ya Madawa ya kulevya, Karim Banji, amesema kuwa ni siku moja toka
Ray C apelekwe katika kituo hicho.
“Kweli
jana tumempokea Ray C, na kusema kweli kwa sasa siwezi zungumzia
maendeleo yake kwa sababu ni siku ya kwanza, lakini leo mchana amekula
vizuri na nimemuacha amepumzika,” alisema Karim.
Pia alisema bado hajajua Ray C atakaa kwa muda gani ndani ya sober house.
“Kusema
kweli mgonjwa akiletwa hapa, atapimwa afya na baada ya hapo anawekwa
katika chumba maalum kwa siku tatu ili aweze kukabiliana na hali ngumu,
na baada ya hapo ataendelea na matibabu ya kawaida, kwa hiyo kikubwa ni
kuombea tu,” alisema Karim.
Chanzo Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni