Mshambuliaji raia wa
Zambia Obrey Chirwa amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea klabu ya
Yanga.
Chirwa ambaye alikuwa anaichezea klabu ya FC Platinum ya Zimbabwe, amewasili leo jioni jijini Dar na kukamilisha taratibu za usali na sasa Yanga imeshakamilisha idadi ya wachezaji saba wa kimataifa kwa mujibu wa kanuni na sheria za TFF.
Nyota huyo anaungana na wachezaji wengine waliowahi kuichezea FC Platinum Donald Ngoma na Thaban Kamusoko ambao walisajiliwa msimu uliopita.

Klabu ya FC Platinum imethibitisha pia nyota huyo kujiunga na Yanga kwa
kuandika ujumbe kwenye akaunti rasmi ya klabu hiyo uliosomeka: “Obreu
Chirwa amejiunga rasmi na klabu ya Young Africans ya Tanzania kwa
mkataba wa muda mrefu. Kila laheri kwenye safari yako mpya,” huo ni
ujumbe ulioandikwa na klabu ya Chirwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni