.

.

02 Mei 2015

RASMI JKT RUVU WAKWEPA KUSHUKA DARAJA, WAIGONGA MGAMBO MKWAKWANI


GOLI pekee la Ally Bilal ‘Benzema’ mapema dakika ya 12’ kipindi cha kwanza limewapa JKT Ruvu pointi tatu muhimu dhidi ya Mgambo JKT katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyomalizika jioni hii uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga.
Kikosi hicho cha Fred Minziro kimefikisha pointi 31 baada ya kushuka dimbani mara 25 na sasa kimebakisha mechi moja dhidi ya Simba.
Kwa mazingira hayo JKT Ruvu ambao wamepanda kutoka nafasi ya 8 mpaka ya sita wamejikwamua kutoka mstari mwekundu wa kushuka daraja.

Mgambo JKT wameendelea kuwa na pointi zao 28 baada ya kucheza mechi 25 na sasa wamebakiwa na mechi moja dhidi ya Azam fc itayopigwa mei 9 mwaka huu uwanja wa Azam Complex, Dar es salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni