.

.

30 Mei 2015

UKATILI WA POLISI MAREKANI KWA WATU WEUSI

Mbeyafm Redio's photo.

Video mpya inayowaonyesha polisi wawili wa Marekani wakimsukuma chini mwanamke mjamzito mwenye asili ya Kiafrika huku mikono yake ikiwa imefungwa nyuma ya mgongo wake imeamsha hasira na maandamano katika mji wa California. Video hiyo iliyotolewa na shirika la haki za binadamu la American Civil Liberties Union Foundation imeenea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii na kupokelewa kwa radiamali kali na Wamarekani weusi pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu.
Tukio hilo limejiri huku kukishuhudiwa ongezeko la vitendo vya udhalilishaji na ukatili vya polisi weupe dhidi ya Wamarekani weusi. Tayari vijana kadhaa wa Marekani wenye asili ya Afrika wameuawa bila hatia mikononi mwa polisi weupe mwaka huu suala linaloonyesha kuendelea ubaguzi wa rangi katika nchi ambayo inajigamba kuwa na eti rekodi nzuri ya uadilifu na usawa kwa watu wote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni