.

.

16 Julai 2016

MAANA YA PAROLE


Parole ni utaratibu wa kisheria unaompa fursa mfungwa aliyehukumiwa kutumikia kifungo gerezani cha miaka minne na kuendelea kutumikia sehemu ya kifungo chake katika jamii kwa masharti maalum baada ya kukidhi vigezo na matakwa ya sheria ya Parole Na. 25/1994. Sambamba na kanuni za Bodi za Parole zilizoandaliwa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali tarehe 29 Agosti, 1997 (GN. 563/1997)(magereza.go.tz/…/vite…/legal-prisons-affairs/parole-services) hivyo kuwezesha Sheria hiyo kuanza kutumika rasmi.
Pamoja na malengo ya Parole yalioainishwa mfungwa anapaswa kukidhi mambo yafuatayo :-
i). Awe ametumikia theluthi (1/3) ya kifungo chake na kuonesha mwenendo wa kurekebika kurudi katika jamii kumalizia sehemu ya kifungo chake kwa masharti maalum. Masharti hayo ni:
• Kuwa chini ya uangalizi maalum kuhakikisha kuwa hatendi kosa lolote mpaka atakapomaliza kifungo chake.
• Kuzingatia masharti ya Parole anayopewa kikamilifu
• Kuwa raia mwema na kuishi kwa kujipatia kipato halali katika jamii.
ii). Awe ameonesha kujutia kosa, kurekebika tabia na kuonesha mwenendo mzuri gerezani.
iii). Mamlaka husika kujiridhisha kuwa hatahatarisha usalama wa jamii.
Kwa upande mwingine Parole ni moja kati ya adhabu mbadala na imeonesha mafanikio makubwa katika nchi nyingi duniani. Utaratibu huu ni wa kipekee kwa kuwa unawagusa wafungwa wa vifungo virefu ambao ndio wengi waliopo magerezani. Aidha, ni utaratibu unaoshirikisha jamii katika urekebishaji kwa kuzingatia usalama wa jamii na dhana kwamba uhalifu ni zao katika jamii.
Kila la Heri Comrade Augustino Lyatonga Mrema naamini Bodi ya Parole utaitendea haki.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni