.

.

25 Juni 2015

UYOGA HUPUNGUZA UNENE


Mbeyafm Redio's photo.
Uyoga unatumika nchini Uchina kama dawa ya kupunguza unene.
Kwa miaka na mikaka, uyoga umekuwa ukitumika nchini humo kama dawa ya kupunguza unene katika wanyama, hayo yamesemwa na watafiti nchini Taiwan.
Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la mawasiliano ya mazingira unabaini kuwa madini ya Ganoderma Lucidum iliyoko ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani mkubwa kwa kutatiza bakteria ndani ya utumbo.
Watafiti wanapendekeza kuwa uyoga hatimaye utatumika katika matibabu ya kupunguza uzito.
null
Madini ya Ganoderma Lucidum iliyoko ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani
Wataalam wanasema kuwa sayansi hiyo ni nzuri, lakini kuweka maji yanayotokana na uyoga kwenye mikebe ya cola hakutawasaidia watu kupunguza uzani.
G. lucidum imekuwa ikiuzwa tangu jadi kama kichocheo cha "kiafya na kurefusha maisha" hayo ni kwa mjibu wa watafiti katika chuo kikuu cha Chang Gung.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni