.

.

20 Septemba 2015

FAHAMU KUHUSU UVIMBE KWENYE OVARI KWA MWANAMKE-2


Wiki jana tulianza kupeana elimu ya kutusaidia kufahamu juu ya tatizo la uvimbe kwenye ovari za mwanamke. Tuliangalia umuhimu wa ovari na kazi zake pia tukagusia kwamba kama ovari hazitakuwa katika ubora wake ni rahisi mwanamke kukosa mzunguzo bora wa hedhi. Leo tutaendelea na kuziangalia aina mbalimbali za uvimbe katika ovari za mwanamke kabla hatujajua sababu ni nini za uvimbe huo.
Kuna aina nyingi za uvimbe kwenye mayai ya mwanamke lakini aina hizi saba ndiyo huonekana sana kwa wanawake wengi ambazo ni;•Follicular cyst – Aina hii ya uvimbe hutokea wakati ovulation isipotokea au baada ya corpus luteum kuanza kusinyaa na kupotea yenyewe baada ya kutokupachikwa kwa yai kwenye kuta za mfuko wa kizazi. Uvimbe huu unakuwa na wastani wa 2.3 inchi kwa upana.
Upasukaji wa uvimbe huu husababisha maumivu makali sana katikati ya mzunguko wa hedhi yaani siku ya ovulation. Maumivu haya yanayojulikana kama mittelschmerz huonekana kwa wanawake robo moja wenye aina hii ya uvimbe. Kwa kawaida, uvimbe huu hauna dalili zozote na hupotea wenyewe baada ya miezi kadhaa.
•Cystedenoma - Ni aina ya uvimbe unaotoka kwenye tishu za ovari na hujazwa na majimaji aina ya kamasi. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa sana hata kufikia inchi 12 au zaidi kwa upana.
•Endometriomas /Endometrial Cysts - Husababishwa na uwepo wa aina mojawapo ya kuta za mfuko wa kizazi unaojulikana kama endometrium kwenye mayai ya mwanamke (ovari). Huathiri wanawake walio katika umri wa kushika ujauzito na huambatana na maumivu sugu ya nyonga (chronic pelvic pain) wakati wa hedhi. Uvimbe huu unakuwa na damu ya rangi ya nyekundu kahawia (reddish brown) na ukubwa wake ni kuanzia 0.75-8 inches.
•Polycysitic appearing cyst - Uvimbe wa aina hii unakuwa ni mkubwa sana na huwa umezungukwa na vijivimbe vingine vidogovidogo na huonekana hata kwa wanawake wenye afya njema au wale wenye matatizo ya homoni.
•Dermoid cyst - Uvimbe huu ambao siyo saratani pia hujulikana kama mature cystic teratoma, huathiri wanawake wadogo walio katika umri wa kushika mimba na huweza kukua na kufikia inchi 6 kwa upana na ndani yake huweza kuwa na mchanganyiko wa nywele, mfupa, mafuta na cartilage. Uvimbe wa aina hii huweza kuwa mkubwa zaidi (inflamed) au kujizungusha (torsion) na hivyo kuathiri usambazaji wa damu kwenda kwenye uvimbe huu na hivyo kusababisha maumivu makali sana maeneo ya tumboni.
•Hemorrhagic cyst - Uvimbe huu hutokea wakati kukiwa na uvujaji wa damu ndani ya uvimbe wa aina yoyote ule ambao umeshajitengeneza tayari. Huambatana na maumivu makali kwenye upande mmoja wa ubavu wa mwanamke (kushoto au kulia).
•Corpus Luteum cyst - Kutokana na kutopachikwa kwa yai la uzazi lililorutubishwa na mbegu ya kiume kwenye mfuko wa kizazi, corpus luteum husinyaa na kupotea yenyewe, aghalabu inaweza kutokea corpus luteum ikajaa maji na hivyo kusababisha uvimbe wa aina hii. Kwa kawaida, uvimbe huu huonekana kwenye upande mmoja (kushoto au kulia) wa mwanamke na hauna dalili zozote zile.
Baada ya kuziangalia aina za uvimbe katika ovari za mwanamke nikukumbushe tu kuwa Sigwa Herbal Clinic ni mabingwa wa kutatua matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi wa mwanamke na mwanaume unaweza ukawatembelea katika vituo vyao. Njombe, Singida, Dar es Salaam, Moshi, Tanga, Mwanza, Mbeya, Arusha, Kahama, Kigoma, Dodoma na Morogoro.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni