Mahali anapo lala kijana Emanuel Fedrick (20)Mkazi wa Mwambeja Kata ya Ilemi jijini kwa zaidi ya Miaka 11 sasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuficha aibu ya familia. |
Na EmanuelMadafa,Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili, amegundulika kufungiwa ndani kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi Jijini hapa.
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amejulikana kwa jina la Fredrick Emmanuel ametajwa kuwa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wake .
Mmoja wa majirani ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kuwa Kijana huyo licha ya kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo vya mikono na miguu,pia amezaliwa akiwa na utindio wa ubongo hali inayomfanya kushindwa kuongea.
Amesema wazazi wa mtoto huyo wamekuwa wakimfungia ndani ambapo hata wao hawakuluhusiwa kuingia ndani ya nyumba hali iliyowafanya washituke na kutoa taarifa ili kumuokoa kijana huyo.
Akizungumzia tukio hilo , Mwenyekiti wa mtaa wa Mwambenja, Rosemary Jama, amesema taarifa za Ferdrick kuishi ndani ya nyumba hiyo walikuwa nazo lakini hawakuwahi kupata taarifa za kwamba kijana huyo hatolewi nje.
“Sisi tunafahamu ndani ya nyumba ya Emmanuel kuna mtoto ambaye ni mlemavu lakini hatukuweza kufahamu mazingira anayoishi kijana huyu, nimeshuhudia kweli huu ni unyanyasaji wa kijinsia, licha ya kutotolewa nje lakini kijana huyu anaonekana amekosa chakula,”alisema.
Akizungumza huku akionesha kutojali , Baba wa kijana huyo Emmanuel John , anasema mwanae Fedrick, alizaliwa mwaka 2007 ukiwa ni uzao wake wa kwanza katika familia hiyo na akufuatiwa na wenzake watatu ambao wote mungu amewajalia na kuzaliwa wakiwa wazima.
Kufuatia tukio hilo baadhi ya majirani wameomba mamlaka husika kuingila kati ili kumsaidia kijana huyo kwani maisha yake yapo hatarini kutokana na wazazi kutoonesha kujali .
Mwisho
Imeandaliwa na Mtandao wa kijamii wa JamiiMojablog-Mbeya na Mtandao wa FahariNews0759-406070,0712199378.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni