.

.

22 Septemba 2015

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM DR MAGUFULI AHIDI KUWATUMIKIA WATANZANIA

Mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi CCM Dr John Pombe Magufuli amewaambia watanzania kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuwatumikia watanzania na kuwataka watendaji wanaotoa taarifa za uongo kwa viongozi waandamizi kuacha tabia hiyo kwa kuwa anazifahamu vyema changamoto na shida za watanzania.
Dr Magufuli ameyasema hayo katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera wakati akihitimisha ziara ya kampeni ya kusaka ridhaa ya watanzania kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kuongeza kuwa ameamua kutumia usafiri wa barabara ili kujionea na kuzifahamu changamoto za wananchi hasa wa hali ya chini ili aweze kuzitatua na kuwatahadharisha watendaji wanaotoa taarifa za uongo lakini pia akaongeza kuwa serikali yake endapo itapata ridhaa ya watanzania imejipanga kuligeuza eneo la Ngara kuwa eneo la kimkakati kibiashara kutokana na jiografia yake na uwepo wa madini aina ya  nikel.
Aidha Dr Magufuli ameendelea kusisitiza kutumia vyema na kwa uadilifu rasilimali za nchi ili kufufua na kujenga viwanda vitakavyosaidia kupunguza tatizo la ajira hususani kwa vijana na kuwa na nchi inayotegemea uchumi wa viwanda.
Dr Magufuli amehitimisha ziara za kampeni katika mkoa wa Kagera ambapo amefanya mikutano katika maeneo ya Misenyi, Kayanga, Kyerwa na hatimae Ngara achilia mbali mikutano ya barabarani alikokuwa akisimamishwa na wananchi huku kiongozi wa msafara alhaji Bulembo akizungumzia kero ya uwepo wa vizuizi vingi barabarani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni