Naibu spika wa bunge
la jamhuri ya muungano wa Tanzania, dk. Tulia Akson amenusurika kifo
baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali Kiwira mkoani hapa.
Dk. Tulia alipata ajali hiyo baada ya gari alilokuwa akitumia
kusafiria kugongana na gari dogo lililokuwa na abiria sita wa familia
moja katika eneo hilo la Kiwira
Taarifa zinasema hakuna kifo kilichotokea kutokana na ajali hiyo
japokuwa majeruhi wengi ambao ni watoto wanne walipatikana katika gari
lililogongana na gari la mhe. Naibu spika.
Naibu spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, dk. Tulia
akson alikuwa akitokea hapa jijini Mbeya ambapo alikuwa na ziara binafsi
katika shule ya sekondari ya wasichana ya Loleza ambapo alisoma elimu
yake ya kidato cha kwanza hadi cha nne kati ya mwaka 1991 hadi 1994.
Katika ziara hiyo naibu spika tulia akson alitoa msaada wa pesa za
kitanzania milioni 5 kwaajili ya ukarabati wa bweni alilokuwa akilitumia
wakati akisoma shuleni hapo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni