Wanajeshi wa AU Somalia
Vikosi
vya serikali ya Somalia vikishirikiana na wanajeshi wa AU wameukomboa
mji wa Merca kutoka kwa wapiganaji wa Alshabab ambao waliuteka mji huo
siku ya ijumaa,kulingana na wakaazi.
Umoja wa
Afrika siku ya ijumaa ulikataa kwamba mji huo ulikuwa umetekwa na
alshabab,ukisema wanajeshi wake waliondoka kwa mkakati.
Al-Shabab
ililazimishwa kuondoka katika mji wa Mogadishu mwaka 2011 lakini
linaendelea kudhibiti maeneo makubwa ya kusini mwa Somalia.
Mwanajeshi
mmoja wa Somalia ameliambia shirika la habari la AFP kwamba vikosi vya
Somalia vikishirikiana na vile vya Umoja wa Afrika vilichukua udhibiti
wa mji wa Merca na kwamba hali imerejea tulivu.
Alashabaab
Kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi ,lakini wapiganaji hao wametoroka.
Amesema kuwa wapiganaji kadhaa wa Alshabaab na mwanajeshi mmoja wa Somalia waliuawa katika vita hivyo.
Mkaazi mmoja pia ameiambia AFP kwamba raia wanne wamefariki katika eneo hilo.
Mapigano
hayo yanajiri wiki tatu baada ya alshabab kuishambulia kambi moja ya
wanajeshi wa Kenya mjini el Ade na kutangaza kuwa wamewaua zaidi ya
wanajeshi 100. BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni