.

.

23 Aprili 2016

Y.W.C.A WATEMBELEA KITUO CHAKULELEA WATOTO YATIMA AMANI KILICHOPO NSALAGA UYOLE.

                                      Rais wa Y.W.C.A RosemaryMabagala  (KULIA)na
                      Mchungaji Bahati Pangani(KUSHOTO)(Picha na Anangisye Essau)
               Mlezi wa kituo cha kulele watoto yatima na wasio jiweza Amani                                         Mchungaji Bahati Mshani Pangani(Picha na Anangisye Essau)



                               
Mwenyekiti wa Y.W.C.A Mbeya Mjini Oliver Kibona
                                       Afisa miradi wa Y.W.C.A Elly Bonke
Afisa miradi wa Y.W.C.A Elly Bonke akiwa na watoto wakituo cha Amani


                       Mwakilishi wa watoto wanaolelewa katika kituo cha Amani Nsalaga Uyole
                                                Picha ya pamoja(picha na Anangisye Essau)

Kituo cha kulelea watoto yatima na wasio jiweza Amani kilichopo Nsalaga Uyole ambacho kinasimamiwa na Mchungaji Bahati Mshani Pangani,kilianziswa mwaka 2006 kikianziswa na umoja wa Wanawake na watoto wa kanisa la moravian Tanzania Jimbo la kusini magharibi,na walianza wakiwa na watoto 45 wote wakiwa shule ya msingi,mpaka sasa kituo kinawatoto 250 wakiwa wanatoka maeneo mbalimbali,mbeya vijijini,pamoja na wilayani,Umalila,wilaya ya Mbozi na wilaya ya Chunya,huku wakishughulikia mambo ya kisaikolojia,afya,pamoja na elimu kwa watoto.
Katika upande wa changamoto zilizopo katika kituo ni baadhi ya wazee na walezi kuwakatalia watoto hao wasipate elimu ili wawasaidie kulima,kuchunga mifugo pamoja na shughuli mbalimbali.

Mwakilishi wa watoto hao ambaye alisema kwa niaaba ya wenzake aliweza kuwashukuru Y.W.C.A n a kusema pia mungu awabariki kwa vitu walivyovileta wao wanaweza kuviona vidogo lakini kwao ni vikubwa na kusema kwamba maneno ya mungu wanasema kwamba Yeyote atakaye wagusa watoto na kuwafadhili agusa mboni ya jicho la mungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni