Aliyekuwa kamanda wa
polisi mkoa wa Mbeya, SACP Ahmed Msangi jioni ya leo ameagana na
wanambeya pamoja na staff nzima ya Redio Mbeya Fm ya jijini Mbeya
kupitia kipindi cha TABARADI na kueleza tathmini ya ya kazi aliyoifanya
kwa kipindi cha miaka miwili na miezi mitatu.
Kamanda
huyo ameeleza kuwa uhamisho wake kwenda mkoani Mwanza ni wa kawaida kwa
jeshi la polisi Tanzania ambapo anabadiliwa na aliyekuwa kamanda wa
polisi mkoani Mwanza ACP Justus Kamugisha .
Ahmed
Msangi ameeleza kuwa kati ya changamoto kubwa kwa jeshi la polisi
katika kipindi chake alichohudumu kama kamanda wa polisi ni matatizo ya
raia kujichukulia sheria mkononi na kusababisha mauti kwa watuhumiwa wa
makosa mbalimbali ambapo kwa mkoa wa Mbeya matukio hayo hujitokeza mara
kwa mara kwa watu wanahisiwa kuwa ni washirikina, wezi na majambazi na
makundi mengineyo.
Pamoja
na hayo kamabda Ahmed Msangi anaingia katika kumbukumbu ya kuwa kati ya
makamanda wa polisi wa mikoa waliofanikiwa kujenga ushirikiano mzuri na
wananchi na kufanikisha kupambana vema na changamoto za
usafirishaji/matumizi ya madawa ya kulevya na bidhaa za
magendo,uhamiaji haramu,uhujumu nyara za serikali,upigwaji wa nondo na
pombe haramu pamoja na mengi.
Pamoja na
hayo amewashukuru wakazi wa Mbeya waliotoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi katika kipindi chote, vyombo vya habari na idara mbalimbali na
kisha ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Mbeya kuupenda mkoa wao,
kushiriki vema katika kuulinda kwa namna zote na kushirikiana na vyombo
vya dola ili kuumbua uhalifu katika jamii na pia amewataka kutoa
ushirikiano na kamanda mpya wa polisi mkoa wa Mbeya, ACP Justus
Kamugisha kwani anaamini ataweza kufanya kazi vema pengine hata kushinda
yeye.
SACP
Ahmed Msangi alianza kuhudumu kama kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
mwishoni mwa mwaka 2013 baada ya kamanda aliyekuwepo Diwani Athumani
kuhamishiwa makao makuu. FICHUO BLOG,CHAMBUZI NEWS na Mbeya fm Radio inamshukuru kwa
ushirikiano wake katika kipindi chote alipokuwa akihudumu kama kamanda
wa polisi mkoa wa Mbeya.
CREDIT FICHUO TZ
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni