Takaribani askari 500 wa Jeshi la Marekani walijiua mwaka jana na
hivyo kuendeleza mkondo wa idadi kubwa ya wanajeshi wanaojiua nchini
humo katika kipindi cha miaka saba iliyopita.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, katika ripoti yake ya
Ijumaa ilisema askari 265 walio katika vikosi vya anga, bahari, nchi
kavu na kikosi cha marine walijiua mwaka 2015. Aidha askari 210 wa ziada
katika jeshi la Marekani walijiua mwaka jana.
Mwaka 2001 wanajeshi 145 walijiua katika Jeshi la Marekani na idadi hiyo imekuwa ikiongezeka kila mwaka.
Msemaji wa Pentagon Luteni Kanali Hermes Gabrielle amesema kuzuia
vitendo vya wanajeshi kujiua ni suala linalopewa kipaumbele na Jeshi la
Marekani.
Kitendo cha Marekani cha kuzikalia kwa mabavu Iraq na Afghanistan na
harakati zake za kichokozi kwingineko duniani si tu zimeleta madhara na
hasara kubwa kwa nchi zinazolengwa, lakini zimesababisha pia matatizo
makubwa ya kiroho, kinafsi na kisaikolojia kwa wanajeshi vamizi wa
Marekani na bila shaka madhara hayo yatadumu kwa muda mrefu kwa
wanajeshi hao na kwa jamii nzima ya Marekani.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni