.

.

06 Aprili 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUTOFANYA KAZI KWA MAZOEA WILAYANI KYELA.


        Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Mkala akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyela  Bi Thea Ntara Bandari ya itungi ziwa Nyasa Kyela.
     Wananchi wa Wilaya ya Kyela walioudhuria kwa ajili ya kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.[Picha na Anangisye Essau]
 
 Na Anangisye Essau Kyela-Mbeya
Mkuu wa mkoa wa mbeya Amos Makala amefanya ziara wilayani kyela na kuweza kutembelea bandari ya itungi port ambako kunaujezi wa meli tatu ambapo moja ni ya abilia mbili ni za mizigo lakini pia alizungumza na madiwani,watumishi wa ,wazee marufu,viongozi wa dini ,na viongozi wa vyama wilayani hapa katika ukumbi wa halmashauri.
Huku akimtaka meneja ya bandari ya Itungi bwana Ntetema Salama kukamilisha meli hizo tatu zinazotengenezwa kwa muda alioutaja na si vinginevyo.

Hata hivyo mkuu huyo aliwaomba watumishi na wananchi kumpa ushirikiano ili kuweza kuiletea maendeleo wila ya na mkoa kwa ujumla ili kuzitatua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi ,pia aliwataka watumishi wa serikali ya wilaya kutoa huduma za hali ya juu kwa wananchi.

Aidha watumishi wa wilaya ya kyela wametakiwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea bali kila mtu anapaswa kuwajibika kwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwaletea tija wananchi kwenye maeneo yao.
Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla alipokuwa akizungumza na baadhi ya Watumishi wa wilaya ya kyela waliojitokeza katika ziara yake ya kwanza wilayani hapa.
Makalla alisema kila mtumishi akiwajibika katika eneo lake litachangia kuondoa ombwe katika uongozi ambapo kila mwananchi atapata huduma katika ngazi husika ili kuondoa maandamano ya wananchi kudai haki na kutaka kero zao zitatuliwe na Mkuu wa Mkoa.

“Nimekuja hapa kwa lengo la kukumbushana sina jipya kinachotakiwa ni uwajibikaji, tuwatumikie wananchi wetu, haiwezekani suala dogo mtu anafunga safari kwenda kwa Mkuu wa Mkoa nataka masuala ya Mkuu wa Mkoa yawe na hadhi ya Mkuu wa Mkoa” alifafanua Makalla.
Alisema ili kuepusha kukaa na matatizo ya wananchi pamoja na migogoro inayoweza kutatulika ni lazima kila Mkuu wa Wilaya pamoja na wataalam wake kutenga siku moja ya kukaa ukumbini kusikiliza shida mbali mbali za wananchi ili zinazoshindikana anapeleka mbele.
“Naagiza kila alhamisi kuanzia saa nne asubuhi hadi saa nane mchana Mkuu wa Wilaya pamoja na wataalam wako mtakaa ukumbini ili kusikiliza na kujibia shida za wananchi kabla taarifa haijafika kwangu” alisema Mkuu wa Mkoa.
Aliongeza kuwa Watumishi wanaojihusisha na mitandao ya kijamii muda wa kazi wanapaswa kujirekebisha kwani hatakuwa mvulimivu kwa mtu yoyote ambaye atashindwa kutimiza wajibu wake kwa jamii.
Mbali na hayo Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza watumishi wote kuhakikisha wanasimamia usafi wa mazingira ili ugonjwa wa kipindupindu usijirudie kyela.
Hata hivyo mkuu huyo aliwataka watendaji wa vijiji kusoma mapato na matumizi kwa wananchi bila ya kupindisha ili kuuondoa kero,ameongeza kuwa swala la madawati kwenye shule zetu liwe limekoma kufikia tarehe 31/5/2016 huku akiwataka madiwani kujitaidi kuhamasisha upatikanaji wa madawati na kusema kuwa wao kama serikali inawategemea sana madiwani na swala hili halina itikadi za vyama.

Makala ametumia nafasi hiyo ya kuwataka mafisa ogani kwenda vijijini kutoa elimu licha ya pembejeo kuja kidogo lakini ziwafikie walengw, amesema kuna vijana wanakaa vijiweni ni swala ambalo ameagiza halmashauri kutenga mapato ya ndani asilimia tano kwa vijana asilimia tano kwa akina mama ili wakopeshwa na waweze kujishughulisha na swala lisianagalie itikadi za vyama.

Pia makala amesema meli zikikamilika uchumi wa kyela utakuwa kwa kasi kubwa sana kwani mizigo mingi itasafirishwa kupitia meli hizo na tayari meli moja itaanza mwezi wa nane mwaka huu na nyingine mwezi wa kumi na nyingine mwakani mwezi wa pili na kuwataka wananchi wa kyela kutumia fursa hizo kwa kufanya biashara.

Na swala la mwisho Amesema kuwa swala la mkuu wa wilaya la kuhusiana na madiwani wasameheane na wagange ya jayo kwani kama hakuna mahusiano mazuri kati ya ofisi ya Dc na madiwani maendeleo hayata enda mbele hata hivyo amemwagiza mkuu wa wilaya Thea Ntara kuwa hataki kusikia tena kipindupindu na kusema kila mwananchi awe na choo.
Huku mkuu wa Mkoa huyo akitaja namba yake ya simu ya mkononi  kwa wananchi   ambayo ni  0763444455akiwataka wampigie au wamuandikie kwa sms yani ujumbe mfupi wa maneno kwa kero zinazojitokeza katika wilaya ya Kyela

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni