.

.

23 Aprili 2016

MKUU WA WILAYA YA MBEYA MJINI AWATIA MOYO WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA KATIKA MAHAFALI YA TISA 2016 SEKONDARI YA IVUMWE MBEYA.

 
                           Mkuu wa shule ya sekondari Ivumwe Emirry.P.Muhondwa


   



                                     

                                    Wanafunzi wa kidato cha sita shule ya sekondari Ivumwe
                                                 [pcha na Anangisye Essau]
 
RISALA YA WANAFUNZI WA KIDATO CHA SITA 2016 KWA MGENI RASMI

 Ndugu mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini,wageni waalikwa,mkuu wa shule,waalimu na wafanyakazi wa shule ,ifuatayo ni risala ya wanafunzi wa kidato cha sita kwa mgeni rasmi.
 Ndugu mgeni rasmi awali ya yote tunamshukuru mungu aliyeweza kufanikisha safari hii ya masomo yetu kwani tulianza mwaka 2014 tukiwa wanafunzi 125 na leo tunahitimu wanafunzi 115idadi hii imepungua kutoka na matatizo mbalimbali moja wapo ikiwa ni ukosefu wa ada.kwa muda tulioka hapa shuleni mafanikio tuliyoyapata nikama ifuatavyo:
Ndugu mgeni rasimi tulifanikiwa kuongoza mtihani wa wa joint kwa kushika nafasi kwanza unaompima mwanafunzi kuingia kidato cha sita unaohusisha baadhi ya shule za wazazi mkoa wa Mbeya na shule nyingine za serikali.
Ndugu mgeni rasmi pia tumefanikiwa kuongoza mtihani wa utamilifu"mock"mikoa mitatu yaaniMbeya,Rukwa,na Katavi kwa kushika nafasi ya kwanza kikanda kutokana na juhudi zetu na jitihada za walimu katika ufundishaji kwa kujitolea muda wao wa ziada.
Ndugu mgeni rasmi,katika matokeo ya kitaifa ya kidato cha sita ya mwaka 2015 shule yetu ilishika nafasi ya kwanza kimkoa kati ya shule 25 zilizopo mkoani mbeya na ilishika nafasi ya 5 kitaifa.hii imetokana na juhudi na bidii kati ya mkuu wa shule,waalimu pamoja na wafanyakazi kwa hilo tunajivunia sana shule yetu ya Ivumwe.
Ndugu mgeni rasmi popotepalipo na mafanikio hapakosi changaomo nazo ni kama ifuatavyo


Ndugu mgeni rasmi katika shule yetu kuna uchakavu wa baadhi ya vyumba vya madarasa kwani baadi ya vyumba vya madarasa sakafu zimeharibika na baadhi ya madara hayana ceilingboard ambapo husababisha uhafifu wa usikivu wakati wa mvua hivyo kupelekea vipindi kuahiriswa.
Ndugu mgeni rasmi uongozi wa shule umejitaidi kuhakikisha  kuwa kuna waalimu wa kutosha kwa mosomo yote .pia na uwepo wa vitabu vya kutosha vya kiada na ziada vinavyokidhi idadi ya wanafunzi.lifuatalo ni ombi ambalo litafanikisha utolewaji wa elimu bora zaidi ambalo ni tunaomba utusaidie kufanikisha ukarabati wa vyumba vya madarasa na sakafu pamoja ceilingboard.
Ndugu mgeni rasni tunashukuru kwa ujio wako kwa kuacha shughuli zako za ujenzi wa taifa na kushiri pamoja nasi katika sherehe hii mungu akubariki.
                            
                                              TAARIFA YA SHULE









Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini awatia moyo wanafunzi wa kidato cha sita katika sekondari ya Ivumwe,hayo aliyasema wakati akiwatunuku vyetu vya kuhitimu huku akiwataka wanafunzi hao,
Mwisho mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini aliweza kuwasisitiza wanafunzi hao kufanya vizuri katika masomo yao na si kuishia tu kidato cha sita,na akionesha baadhi ya mifano hai ambayo ipo katika jamii yetu inayotunzunguka,pamoja kuwasisitiza kuwa na malengo ya kile kitu unachokitaka na kama unataka division one lazima uwe na malengo nayo pamoja na kuitafuta hiyo one,huku akiwasihi kupenda masomo na si kuwachukia waalimu kwani ukimchukua mwalimu hata somo lake hutolipenda,na kila kitu kuweza kufanya kitu kwa malengo
kwa upande mwingine mkuu huyo wa wilaya amewahaidi waalimu pamoja na wanafunzi wano baki shuleni hapo kushugulikia matatizo yote pamoja na changamoto kwa kukaka na wadau wa elimu ndani ya wilaya yake ya Mbeya mjini kwa ajili ya kufanya arambee kwa ajiri ya ukarabati wa mabweni na madarasa,huku akiwatakia mitihani mema,na kusema kwamba wanauwezo wakushika nafasi ya kwanza kitaifa kama wanania yakufanya vizuri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni