Waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano huo wakati wa Meya akitoa tamko la kuwasimamisha watumishi mapema leo Mei 5.2016 katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa. |
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mh.
Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016 ametangaza kuwasimamisha kazi kwa
watumishi wawili wa Manispaa ya Kinondoni, akiweo Mwanasheria Mkuu BW. Burton
Mahenge na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya Madiwani kuamua
kwa kauli moja kuwachukulia hatua hiyo.
Akisoma taarifa na nyaraka mbalimbali
mbele ya wanahabari, Mh. Boniface Jacob alieleza kuwa: Kikao cha Kamati ya
fedha na Uongozi cha tarehe 29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri
yote ambayo hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton
Mahenge, na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na
kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.
“Kufuatia makosa yaliyogundulika katika
mashauri hayo, baraza la Madiwani la terehe 04/05/2016, limeamua
kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa Manispaa Bw. Burton Mahenge,
na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard Chidaga”.
Mh. Boniface Jacob aliyataja Makosa
yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-
1.
Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa. Mkataba huo, ulifanyiwa
marekebisho mbalimbali bila idhini ya Halmashauri na hali hiyo kumpatia
sauti zaidi Mwekezaji na kuamua analotaka.
Manispaa ilipaswa kupata shilingi milioni
900 kwa mwaka katika uwekezaji huo,lakini kutokana na Mgogoro wa
kimkataba mapato hayo hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi billion 4.5
mpaka sasa. Mradi ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote viwili kiwanja
Na.277 na 322 ambapo uwekezaji katika kiwanja namba 277 una nyumba (Apartments)
44 na katika kiwanja Na.322 nyumba 68 (Mwekezaji nyumba 29 KMC Nyumba 17)
2 .Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za
Magomeni Kota.
Manispaa iliandaa mpango wa kuendeleza eneo
la Magomeni Kota , hivyo kuwaondoa wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo kongwe.
Wapangaji walifungua shauri la kupinga kuondolewa katika nyumba, na kutoa madai
ya kujengewa
nyumba,ama kulipwa fedha za fidia
kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hili Mahakama imeruhusu iliamuru
Manispaa kukaana kumalizana na wapangaji nje ya mahakama. Halmashauri
ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa
kila mpangaji kama kodi ya Mwaka na kumpatia kila mpangaji kiwanja.Hivyo Manispaa
inatakiwa kulipa shilingi 3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo,kwa mchanganuo
wa Tshs.695,520,000/= pango la mwaka na Tsh2,576,000,000/=fidia ya viwanja 644.
3.Uwekezaji Eneo la Coco Beach
Oysterbay.
Manispaa iliingia Mkataba wa Q-Consult
Limited. Kampuni hiyo ilishindwa kutekeleza mradi kwa wakati na Manispaa
ikavunja Mkataba huo. Q-consult Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa
vizuri na kwa sababu ya kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo.
Halmashauri iliagiza kukata kwa rufaa lakini hakukuwa na hatua zozote
zilizochukuliwa, na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa na
serikali mwanasheria mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe Magufuli
kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa mwanasheria alikuwa hajakata
rufaa.
4.Mradi wa ujenzi wa maduka Makumbusho
(Eastern Capital LTD)
Katika shauri hili mabadiliko ya mradi
yalifanyika bila idhini ya Halmashauri kwa kubadili michoro na kuongeza maeneo
mengine katika mradi kama vile kituo cha Mabasi , Matangazo na choo.
viwango
vya mgawanyo wa mapato ya Manispaa katika maeneo yaalioongezewa ni kidogo
ukilinganisha na uhalisia.
Halmashauri haina mkataba na mwekezaji
kwa baadhi ya uendeshaji wa majengo ‘above two storey’hazipo kwenye kumbukumbu
za Halmashauri.
Mkataba juu ya ujenzi na uendeshaji wa
stendi hauna manufaa kwa Halmashauri ,KMC inapata 1%ya makusanyo kwa mwaka sawa
na mil.4 tu kwa mwezi wakati kabla ya uwekezaji ,local standy Halmashauri
ilikuwa ikipata 12mil. kwa mwezi.
5.Kubomolewa Kwa Ofisi ya Kata ya
Msasani.
Mwanachi aliyejulikana kwa jina la
Chacha aliingilia eneo la Ofisi ya Kata Msasani na baadae kuishitaki
Manispaa.Usimamizi dhaifu wa shauri hilo ulisababisha mahakama kutoa amri ya
kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri
halisikilizwi na hakuna ufuatiliaji unaoendelea. Hata hivyo bwana Chacha
kwa makusudi aliamua kuuza kiwanja hiki, kwa Lake Oil Co. Limited
wakati shauri halijaisha. Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa
kukamilika kwa shauri hilo.Tangu upandewa pili ulikataa jaji.Tuna zaidi ya
mwaka hatuja pangiwa jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.
6.Ujenzi wa Nyumba za Makazi.
(Apartments ) Hill Road Oysterbay
Mradi unafanyika kwa ubia na Mwekezaji
Texas Enterprise company LTD, Mkataba uliingiwa mwaka 2009, na Mradi umesimama
kwa Muda Mrefu sasa.
Pamefanyika mabadiliko katika Mkataba na
Mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini ya Halmashauri. Manispaa
inakosa manufaa ya Mali yake kwa sababu ya kuchelewa kwa Mradi. Lakini
pia uendeshaji mpya wa sasa hauna makubaliano wa Financial proposal na
Investment capital.
7.
Ujenzi wa nyumba za Makazi(Apartments).Kiwanja Na. 314 Toure Drive.
Mradi huu unatekelezwa kwa ubia na
Kampuni ya Lake Oil Limited. Mkataba uliingiwa 2019. Mabadiliko yamefanyika
katika Mkataba bila Idhini ya Halmashauri na kusababisha Mradi kuchelewa
kukamilika. Manispaa inakosa Manufaa ya Mali yake kwa kuchelewa kukamilika
mradi huu.
Aidha, Mh. Boniface Jacob amesema kuwa,
itakuwa ni jambo la aibu kwa Manispaa kushindwa kuchukua hatua suala la mradi
wa Coco Beach, licha ya Rais Dk. John Pombe Magufuli kutaka eneo hilo
libaki kuwa mali ya wananchi na si kumuachia mwekezaji kuweka miradi yake.
Hata hivyo Mwanasheria huyo wa Manispaa
hakuweza kuchukua hatua yoyote hadi sasa hivyo kuonekana bado mchezo unachezwa
hivyo maamuzi ya kusimamishwa ambapo pia licha ya kusimamishwa, Meya huyo
amebainisha kuwa, atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa mamlaka
husika za Kiserikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni