.

.

11 Aprili 2016

NIMEKUWEKEA PICHA 14 ZA SAFARI YA MAKUMBUSHO YA ISIMILA PAMOJA NA VIDEO YA BAADHI YA MIAMBA (MKOANI IRINGA)









pia kunasehemu kama isimila ambako kuna miamba mizuri na mikubwa yenye kuvutia.







                                                    Iringa isimila.

 Safari ya kuelekea Iringa Isimila ilikuwa jumapili ambapo mhandishi wa mtandao huu alipata nafasi ya kuongozana na watalii waliotoka marekani na kuja Tanzania kwa ajili ya kuangalia mambo mbalimbli ya kitalii katika nchi ya Tanzania,huku safari yao ya kwanza ilikuwa ni kwenye Kimondo kinachopatikana Mkoa mpya wa Songwe Katika wilaya Mbozi,Jumapili hii waliweza kutembelea Isimila na kujifunza mambo mengi,moja ya vitu walivyojifunza pamoja na mhandishi wa mtandao huu juu ya zama za mawe za kale.


                       




Isimila ni eneo la kihistoria lililopo mkoani Iringa nchini Tanzania katika kijiji cha Ugwachanya kwenye kata ya Mseke kilichopo kilomita 20 kutoka Iringa mjini karibu na barabara kuu ya A 104 kuelekea Mbeya. Eneo hili ni kivutio kimojawapo kinachoupamba mkoa huu wa Iringa.
Bonde la Isimila lilikaliwa na watu tangu Zama za mawe za Kale Ni katika eneo hili ndipo zana za mawe za kale na nguzo za asili za Isimila zilipogunduliwa hapo tangu mwaka 1951. Pia ndani ya eneo hili mafuvu na mifupa mingi ilionekana kati yao ilipatikana mifupa ambayo ilifanana na twiga wa hivi sasa, ila tofauti ni kwamba, mifupa hiyo iliashiria kuwa twiga hao walikuwa na shingo fupi, ambapo pia kulikuwa na aina ya tofauti ya viboko.
Zana hizo zinasadikiwa kuwa zilikuwepo tangu miaka laki tatu hadi nne kabla ya Kristo. Miongoni mwa zana zilizopo katika korongo la Isimila ambalo lina mikondo miwili ni pamoja na mikuki iliyotumika kwa ajili ya kujihami na pia mawe ya kombeo kwa ajili ya uwindaji.
Pia vifaa kama nyundo zilizokuwa zikitumika kwa ajili ya kutengenezea zama nyingine na Shoka zilizotumika kwa kazi ya kuvunja mifupa, nyembe na visu.

 Kwa Hisani ya Johson Sailowa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni