.

.

11 Juni 2016

CHUO CHA KILIMO MBEYA POLYTECHNIC COLLEGE CHAFUNGIWA.




Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amosi Makalla akitoka chuoni hapo Mara Baada ya Kukifungia Chuo hicho.(Picha na David Nyembe wa Fahari News)






Vilio kwanafunzi wa chuo hicho vilitawala.


mkurugenzi wa chuo Ellerton Mwamasika akiwa chini ya Ulinzi wa Polisi Mara Baada ya kufungiwa kwa chuo cha
Mbeya Polytechnic


Akiingia kwenye Gari.
Na David Nyembe -Mbeya

Baraza la Elimu ya Ufundi  (NACTE) kupitia Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makalla imekifungia chuo cha kilimo cha Mbeya Polytechnic cha jijini Mbeya ambacho kilisajiliwa na Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) kwa jina la Ilemi Polytechnic mwaka 2012.
Katika taarifa iliyotolewa mbele ya uongozi wa chuo hicho, wanafunzi wa chuo hicho na waandishi wa habari, mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala amesema kuwa sababu za kufungiwa kwa chuo hicho ni pamoja na kutotambuliwa kwa program za kilimo na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kutokana na kutokufuata mchakato wa wizara hiyo ambao pamoja na mambo mengine walitakiwa kuijulisha wizara husika kutambuliwa kwake na NACTE na kukamilisha matakwa ya Wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi kwa taaluma hiyo.
Aidha imebainika kuwa wanafunzi 270 kati ya 359 wa program ya kilimo walidahiliwa kujiunga na chuo hicho pasipo kufuata taratibu na sifa stahiki za za kujiunga na masomo hayo ambapo kati ya sifa hizo ni pamoja na ufaulu mzuri wa masomo ya Kilimo, Fizikia, Baiolojia, Kemia, Hesabu na Jiografia.
Pamoja na sababu hizo lakini pia imebainika kuwa chuo hicho cha Mbeya Polytechnic hakikuwa na waalimu (wakufunzi) wa kutosha au kukidhi ufundishwaji wa moduli zote kwa idadi ya wanafunzi walio dahiliwa, mazingira duni na hafifu ya kusomea wanafunzi, kudahili wanafunzi kwa awamu nne kwa mwaka na hivyo kuwa kinyume na msimu wa mvua kwa mikoa ya nyanda za juu kusini pamoja na akaunti za chuo kumilikiwa na kuratibiwa na familia ya mkurugenzi wa chuo Ellerton Mwamasika na hivyo kushindwa kuwalipa waalimu na hata kushindwa kuwapeleka wanafunzi katika mafunzo ya vitendo.
Hata hivyo mkurugenzi wa chuo hicho Ellerton Mwamasika amekiri kufanya makosa ya kitaaluma katika uongozi wa chuo hicho na kisha kushikiliwa jeshi la polisi mkoa wa Mbeya huku akiamriwa kurejesha gharama zote zilizotumiwa na wanafunzi wa chuo hicho mara moja. Pia mkurugenzi wa chuo hicho Ellerton Mwamasika kwa niaba ya wanahisa wa chuo hicho ametakiwa kuripoti kwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai na kwa mkuu wa polisi wa mkoa ili apewe masharti ya ziada hadi atakapomaliza kulipa madeni yote.
Baadhi ya wanafunzi wameshukuru kusikilizwa na kuchukuliwa hatua ya kufungiwa kwa chuo hicho kwani wamekuwa wakinyanyasika kwa kuongezewa ada kila mara huku wengine wakidai kutopewa vyeti vyao baada ya kumaliza masomo katika chuo hicho na wengine wakilia na madeni wanayodaiwa baada ya kukopa pesa kwaajili ya ada na matumizi mengine ya chuoni.
Pamoja na yote mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makala ametoa rai kwa wananchiwote kuwa makini pale wanapotaka kujiunga na vyuo vya elimu ya kati na juu kuhakikisha wamefanya utafiti wa kutosha kuhusu vyuo husika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni