.

.

12 Julai 2016

HAYA NDIO MANENO AMBAYO NI UFUNGUO WA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.




MWAMINI MUNGU;

Kila mtu atizaliwa kwa mpango wa Mungu kwa hiyo kila Mtu ameletwa duniani kwa sababu fulani. Kila mtu Mungu amempangia kitu kwa ajili ya kusaidia wengine na kujisaidia yeye. Ambacho unakiwaza kukifanya chenye malengo ya kukujenga kimaisha kiroho usikiache kwa sababu hicho ndicho MUNGU amekupa ili kufanikisha maisha yako.

JIAMINI;

Pia baada ya kufikiria cha kufanya kiweke katika matendo amini uwezo wako wa kukitenda achana na watu ambao wanakuambia kwamba huwezi kutimiza ambacho unakitaka au unachokifanyia kazi ili kuweza kutimiza haja za maisha yako. Jiamini pambana kama unataka kusema sema kama unataka kujenga jenga PAMBANA NA MAISHA NA NDOTO ZA MAISHA YAKO JIAMINIIII.



KUWA MVUMILIVU;

Ili mtoto azaliwe lazima mama avumilie uchungu mkali ambao unampata na tambua kwamba hakuna uchungu unaoshinda uchungu wa mwanamke wakati wa kujifungua. Sasa kama yeye ameweza kuvumilia hiyo sasa kwa nini wewe ushindwe kuvumilia hizo changamoto unazozipata katika harakati zalo za kutimiza ndoto zako? MUNGU YUPO NAWE KWA SHIDA NA RAHA VUMILIA UTAFANIKIWA.

TUMIA NAFASI;

Hapa namaanisha kwamba pale ambapo unaona nafasi ambayo unaweza itumia ili kutimiza ulichokipanga sasa amini kwamba hiyo nafasi ni Mungu amekuonesha na pale ambapo utashindwa kuivumilia na kupambana nayo apo itakuwa umeshindwa kutimiza ndoto zako. Heshimu sana nafasi unazozipata kwa sababu hizo ndizo zitakufikisha katika lengo lako.

FANYA KAZI KWA BIDII;

Kitabu cha biblia kinasema asiye fanya kazi na asile kwa hiyo kaa mbali na uvivu na kwa kufanya hivyo utaona unachokipanga kinatimia usipumzike kwa sababu umechoka bali pumzika pale ambapo umetimiza lengo lako ulilopanga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni