Hii ni katika hali ambayo tume hiyo imesema kuwa, matokeo ya awali ya
uchaguzi mkuu uliofanyika siku ya Jumamosi yatatangazwa kesho Jumanne.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amesema uchaguzi wa Nigeria
kwa kiwango kikubwa ulifanyika kwa utulivu na mpangilio wa kuridhisha.
Mkuu huyo wa UN amesema kuna haja kwa Wanigeria kuonyesha ukomavu wa
demokrasia kwa kukubali matokeo yatakapotangazwa. Jumuiya ya Kiuchumi ya
Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS), imetoa kauli kama hiyo na
kusisitiza umuhimu wa kudumishwa amani nchini Nigeria hata baada ya
matokeo ya uchaguzi kutangazwa.
Kiti cha urais kiliwavutia wagombea 14 ingawa mchuano mkali umetajwa
kuwa kati ya Rais wa sasa, Goodluck Jonathan na kiongozi wa zamani wa
kijeshi, Mohammadu Buhari.


Hakuna maoni:
Chapisha Maoni