Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika futari aliyoiandaa kwenye
makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa
mkoa wa Dodoma, Alhaj Adam Kimbisa na Wapili kushoto ni Kaimu Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Ahmed Said.Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Makamu wa Rais, Muungano na mazingira, January Makamba.(Picha na ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John
Malecela katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni
16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Ulanga, Goodluck
Mlinga katika futari aliyoiandaa kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni
15, 2016. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba katika futari aliyoianda
kwenye makazi yake mjini Dodoma Juni 15, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia
Ackson katika fuatari aliyondaa kwenye makazi kake mjini Dodoma Juni 15,
2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………….
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema kila mkoa unatakiwa kuunda Kamati ya Amani
kama njia ya kudumisha amani na utulivu kwenye mikoa yote nchini.
Waziri
Mkuu ametoa wito huo jana usiku (Jumatano, Juni 15, 2016) wakati
akizungumza na viongozi wa dini wa mkoa wa Dodoma na baadhi ya wazee
maarufu wa mkoa huo aliowaalika kwenye futari katika makazi yake mjini
Dodoma.
Amesema
anatambua kuwa mkoa wa Dodoma uko shwari kwa sababu ya mshikamano
uliopo baina viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo. “Nimegundua kuwa
siri kubwa ya mkoa wa Dodoma kuwa na utulivu ni kuwepo kwa kamati ya
amani yenye viongozi mahiri, kwani sote tunatambua kuwa kazi ya viongozi
wa dini ni kuwaimarisha watu kiroho,” alisema.
Waziri
Mkuu alisema ziko nchi zinatamani kuwa kama Tanzania kwa sababu wao
hawana uhakika wa kulala na kuamka salama asubuhi. “Pamoja na yote sisi
tuna uhakika wa asilimia 99 kulala usiku na kuamka salama asubuhi, kwa
sababu ya amani iliyopo,” alisema.
Hadi
sasa mikoa ambayo imekwishaunda kamati za amani ni Dar es Salaam,
Mwanza, Geita, Dodoma, Arusha, Lindi, Mtwara, Tanga na Mbeya.
Akigusia
suala la mauaji ya hivi karibuni, Waziri Mkuu alisema anawaomba
Watanzania kila mmoja kwa imani yake akemee kwa nguvu matendo hayo kwa
sababu yeye haamini kama yamefanywa na Watanzania ambao wamelelewa
kwenye misingi ya dini.
“Siamini
kama kuna mtoto aliyelelewa kwenye misingi ya Uislamu anaweza kuingia
msikitini na kuwaua wenzake wakati wakimwomba Mungu. Na wala siamini
kama kuna mtoto aliyelelewa na kukuzwa Kikristo anaweza kuingia kwenye
nyumba ya ibada akakuta watu wanasali na kuamua kuwaua. Ninawaomba
tukemee kwa nguvu zote tabia hii,” alisisitiza.
Aliwataka
watanzania wote wawe na walinzi wa wenzao kwa sababu kila mmoja ana
jukumu la kumlinda mwenzake. “Tusiachie majeshi kazi hii kwa sababu kila
mmoja na jukumu la kwanza kujilinda yeye mwenyewe na kisha kumlinda
jirani yake,” alisema.
Kwa
upande wake, Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Ahmed Said alisema
wanawaombea dua Mheshimiwa Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu katika
kazi za kuleta maendeleo kwa Watanzania. “Pia tutaendelea kuiombea nchi
yetu ili Mwenyezi Mungu azidishe amani yake na watu wake waishi kwa
amani, upendo na utulivu,” aliongeza.
Naye
Waziri Mkuu mstaafu, Dk. John S. Malecela ambaye alikuwa miongoni mwa
wazee maarufu walioalikwa kwenye futari hiyo aliwataka waalikwa wenzake
waendelee kuwaombea viongozi wa kitaifa na kusisitiza kuwa kila mmoja
ana wajibu wa kuombea amani ya Tanzania ambayo imedumu kwa miaka mingi
iendelee kuwepo.
Katika
hatua nyingine, Askofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania Dayosisi ya
Kati, Askofu Amos Muhagachi, ambaye alipewa fursa ya kutoa salamu fupi
kwenye hafla hiyo, alisema kwenye mkoa huo hakuna magomvi ya kidini kwa
sababu viongozi wa dini zote wanashirikiana kwa karibu sana.
“Hapa
Dodoma Maaskofu tunashirikiana vizuri na Masheikh. Hivi sasa, masheikh
vijana na wachungaji vijana wameanza kuiga haya tunayofanya, na zaidi ya
yote tunashirikiana pia kuwaombea Rais wetu, Makamu wa Rais pamoja na
wewe Mheshimiwa Waziri Mkuu,” alisema
Chanzo Blog ya Wananchi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni