.
31 Machi 2015
HABARI ZILIZOTUFIKIA:MGOMO SONGEA.
Mgomo wa wafanya biashara umeendelea kuchukua sura mpya baada ya wafanya biashara wa daladala mjini Songea kugoma kufanya kazi toka asubuhi kwa madai ya kuunga mkono mgomo wa wafanya biashara unaoendelea katika mikoa mabalimbali nchini ili kushinikiza serikali kumuachilia kiongozi wao Bwana Joseph Minja pamoja na kutatua madai yao ya matumizi ya mashine za EFDS pamoja na ongezeko la kodi kwa asilimia mia moja.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu aliyepo mjini songea hali hiyo imesababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa songea ambao wamelazimika kutembea kwa miguu kwenda maeneo mbalimbali ya mji huo ambapo jeshi la polisi limeimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni