Zoezi la
kuweka mipaka mipya ya mkoa wa manyara na Dodoma mipaka ambayo pia
inadaiwa kusababisha mgogoro wa muda mrefu kati ya kijiji cha KIMOTOROK
na pori tengefu la mkungunero limeshindikana baada ya wakazi wa kijiji
cha KIMOTOROK kulikataa zoezi ilo kwa madai kuwa tume ya wataalam
wanayofanya kazi hiyo hawakushirikishwa na mipaka inayowekwa imeingia
ndani ya kijiji chao hivyo hawapotayari kuona zoezi hilo likiendelea.
Wakizungumza na ITV baada ya kugomea
zoezi ilo na wapimaji kuondoka katika eneo ilo wakazi wa kijiji cha
KIMOTOROK wamesema wameshindwa kuvumilia kuona zoezi hilo likiendelea
huku wapimaji kutoka serikalini wakiendelea kupotosha kwa kuweka mipaka
ndani ya kijiji chao na wananchi wakikatazwa kushiriki na kwamba zoezi
hilo linampango wa kuongeza mgogoro siyo kumaliza.
Mwenyekiti wa kijiji cha KIMOTOR Elias Ormonyo amesema awali
Alipatiwa taarifa kuwa wapima watakuja katika eneo hilo lakini
Walipofika hakushirikishwa na cha ajabu hata yeye mwakilishi wa
Mwananchi htakiwi kujua kinachoendelea hivyo anaunganana
Wananchi kulikataa zoezi hilo.
Mbunge wa simanjiro CHRISTOPHER OLE
SENDEKA ameeleza masikinitiko yake kwa namna zoezi hilo ambalo lingeweza
kuwa utatuzi wa mgogoro kushindikana na kuitaka serekali kuwa makini
inapo tekeleza mipango yenye maslahi kwa wananchi na iwashirikishe
kwakuwa wananchi wanayajui maaeneo yao kuliko mtaalam anayefika kwa mara
ya kwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni