Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Mhe. Philip
Mangula mara baada ya kuwasili kwenye Makao Makuu ya CCM ofisi ndogo,
Lumumba muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha kamati kuu maalum.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipitia ajenda kabla ya kikao kuanza kwenye ukumbi wa NEC ,
Makao Makuu ya CCM ofisi ndogo kulia kwake ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa awamu
ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum
kilichofanyika Ofisi Ndogo Lumumba jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa awamu
ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza pamoja na Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto) pamoja na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu, Spika wa Baraza la
Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada ya kumaliza kikao maalum kwenye
ofisi ndogo za CCM Lumumba jijini Dar es salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
akizungumza na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Maulid na
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dk. Tulia Ackson mara baada
ya kumaliza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM kilichofanyika , Makao
makuu ya CCM, Ofisi Ndogo Lumumba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni