.

.

10 Aprili 2015

BREAKING NEWZZ! JULIO ATIMULIWA COASTAL UNION.





KOCHA wa Coastal Union, Jamhuri Musa Kiwhelo 'Julio' ametyimuliwa baada ya kichapo cha magoli 8-0 alichopata kutoka kwa Yanga jumatano ya wiki hii.
Taarifa za ndani na za uhakika kutoka kwa viongozi wa Coastal, siku hiyo baada ya kipigo walikubaliana kumtimua Julio na yeye alipewa taarifa hizo na kukubali.
Ili kulinda heshima yake, Julio akaomba aongoze mechi ya jumamosi uwanja wa Azam Complex dhidi ya Jkt Ruvu jumamosi ya wiki hii kwa nia ya kuogopa kudhalilishwa.
Baada ya mechi hiyo dhidi ya kikosi cha Fred Minziro, Julio atatimka rasmi na kusubiri kuanza maandalizi ya ligi kuu na timu yake, Mwadui fc.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni