.

.

10 Aprili 2015

MGOMO WA MADEREVA WATIKISA DAR.









MADEREVA wa mabasi ya mikoani na daladala wa jijini Dar leo wamefanya mgomo kupinga agizo la Mamlaka ya Kudhibiti Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (Sumatra) lililowataka kwenda kusoma katika Chuo cha Usafirishaji (NIT).
Mwandishi wetu amezunguka maeneo tofautitofauti jijini Dar na kujionea hali halisi ya mgomo wa mabasi ya mikoani pamoja na daladala za maeneo tofauti ya Jiji la Dar.
Mwandishi wetu pia aliweza kufika eneo la Stendi ya Ubongo na kujionea hali ilivyokuwa asubuhi na kuzungumza na baadhi ya madereva ambao walikuwa na kauli tofautitofati kuhusiana na mgomo huo.
Mmoja wa madereva ambaye alijitambulisha kwa jina la Ally Abdallah Shalon anayefanya kazi zake kati ya Dar es Salaam na Dodoma, alisema kuwa sababu kubwa ya kutokufanya shughuli zake ni kutokana na kikao ambacho walipanga kukifanya leo kujadili agizo la Sumatra lililowataka waende shule kusoma.
Dereva mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Khamis anayefanya shughuli zake kati ya Mwanza na Dar es Salaam alisema sababu iliyomfanya agome ni kupinga sheria mpya ya Sumatra iliyopitishwa na jeshi la polisi kuwataka madereva wote wa abiria (Pasangers Services Vehicle) kwenda kusoma kozi ya miezi miwili kwa gharama ya shilingi laki tano.
Khamisi alisema sheria hiyo inawabana sana madereva kwani moja kati ya vipengele vya sheria hiyo imeeleza kuwa, dereva yeyote atakayekamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi hakuna faini yoyote bali unapelekwa mahabusu kwa muda wa siku kumi na nne baada ya kumaliza siku hizo, anapelekwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.
“Hii sheria inatubana sana, mtu ukihitaji kubadilisha leseni yako ikipitwa na muda unatakiwa kurudia tena kwenda kusoma darasani kwa muda wa wiki mbili kwa ada isiyopungua laki tano na kuendelea kitu ambacho kinatuumiza sisi madereva,” alisema Khamis.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni