Chama cha
Demokrasia na maendeleo ( CHADEMA ) kimemtaka mwenyekiti wa tume ya
taifa ya uchaguzi ( NEC ),jaji mstaafu Damian Lubuva kutangaza tarehe
rasmi ya zoezi la kupiga kura ya maoni kwa katiba inayopendekezwa ili
kuwaondoa wananchi katika hali ya sintofahamu, baada ya zoezi hilo
kuahairishwa kwa muda usiojulikana kutokana na kutokamilika kwa
uandikishaji upya wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Aprili 2
mwaka huu tume ya taifa ya uchaguzi ilitangaza kuahairisha tarehe ya
kupigia kura ya maoni katiba inayopendekezwa iliyopangwa kufanyika
aprili 30, licha ya tume hiyo kuelezwa tangu awali na wadau kuwa
haitawezekana kura ya maoni kufanyika tarehe hiyo kama ilivyokuwa
imetangazwa awali na Rais Jakaya Kikwete.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa baraza la wazee wa chadema wilaya ya ilemela
mhandisi Vedasto Patrick amevitaka vyama vya siasa nchini kusimamia
amani na utulivu uliopo nchini, kwani amani ni zaidi ya jambo lolote na
inahitaji kulindwa na kila mtanzania ili kulinusuru taifa kuingia katika
machafuko yanayotokea hivi sasa katika mataifa mengine.
Kuhusu
mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi – ALBINO yaliyopoteza maisha ya
watu 76 nchini, wakiwemo watu 15 wa mkoa wa Mwanza huku wengine 50
wakiwa wamepoteza viungo mbalimbali vya miili yao, mweka hazina wa
chadema wilaya ya ilemela Edwin Sarungi amesema kuamini kuwa viungo vya
Albino vinasaidia kupata madini, madaraka ya kisiasa pamoja na kuleta
utajiri, ni imani potofu, za kishetani, kifedhuli, kijinga na za kipuuzi
huku mwenyekiti wa Bavicha wilayani humo John Memba akiwahimiza
wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura muda
utakapowadia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni