.

.

16 Aprili 2015

SUMATRA YASHUSHA NAULI ZA MABASI YA MASAFA MAREFU


Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushushwaji wa nauli za mabasi ya masafa marefu ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.

kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Udhibiti usafiri wa barabara,Geffrey Silinda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Mamlaka ya Uthibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) leo jijini Dar es Salaam,kulia ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA),Gilliard Ngewe.


Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii)
Na Bakari Issa,Globu ya jamii.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(SUMATRA) imeshusha nauli za mabasi ya masafa marefu huku nauli za daladala viwango vyake vikibaki kama kawaida.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA),Gilliard Ngewe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es salaam leo.
Ngewe amesema uamuzi huo umekuja baada ya mamlaka hiyo kufanya utaratibu wa kupitia kanuni kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali ikiwemo watoa huduma ili kutoa maoni yao,kutokana na ongezeko la msongamano wa magari mijini.
Viwango vilivyobainishwa kutokana na ukokotoaji wa nauli mpya za mabasi ya mijini ni pamoja na;
0-10km nauli ya sasa ni Sh.400 sawa na asilimia 5.8
11-15km nauli ya sasa ni Sh.450 sawa na asilimia 0.3
16-20km nauli ya sasa ni Sh.500 sawa na asilimia 2.9
21-25km nauli ya sasa ni Sh.600 sawa na asilimia 2.8
26-30km nauli ya sasa ni Sh.750 sawa na asilimia 1
Huku nauli ya Mwanafunzi ikibaki palepale sh.200
Wakati viwango vipya vya nauli za mabasi ya masafa marefu ni pamoja na;
Daraja la kawaida la chini kwa Barabara za Lami ,viwango vipya vilivyoridhiwa ni 34.00 TZS/Abiria/km sawa na 7.8%
Daraja la kawaida la chini kwa Barabara za vumbi ,viwango vipya vilivyoridhiwa ni 42.50 TZS/Abiria/km sawa na 7.8%
Daraja la kawaida la juu, kiwango kilichoridhiwa ni 44.96TZS/Abiria/km
Daraja la kati,viwango vilivyoridhiwa ni 50.13TZS/Abiria/km sawa na 5.81%
Aidha,Bodi hiyo ya Wakurugenzi imeamua kwamba nauli za mabasi ya hadhi ya juu (Luxury bus) hazitadhibitiwa ili kuchochea ubunifu katika utoaji huduma na ushindani kati ya huduma za barabara na njia njinginezo za usafiri.(Muro)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni