Kiongozi wa waasi wa ADF, Jamil Mukulu (menye shati jeupe).
Waasi wa Allied Democratic Forces (ADF).
Raia wakikimbia mapigano dhidi ya ADF.
JEESHI
la polisi nchini limefanikiwa kumtia mbaroni kiongozi wa kundi la
waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) wa nchini Uganda, Jamil
Mukulu, ambaye amekamatiwa nchini Tanzania.
Mukulu
aliyekuwa akiongoza waasi hao katika mauaji wa halaiki katika nchi za
Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) tangu miaka ya 1990,
alikamatwa nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi huu akitokea mashariki mwa
DRC.
Vyombo
vya habari nchini Uganda vimethibitisha kutiwa mbaroni mtu huyo ambaye
kundi lake linatuhumiwa kufanya mauaji ya watu 300 tangu mwezi Oktoba
mwaka jana hadi sasa huko DRC.
Mukulu
ametiwa mbaroni kwa ushirikiano wa polisi wa Tanzania na wenzao wa
Uganda. Hata hivyo, jeshi la Uganda limesema kuwa haliwezi kuthibitisha
kuwa mtu aliyetiwa mbaroni ni Jamil Mukulu hadi atakapofikishwa nchini
humo na kuchukuliwa vipimo vya vinasaba vya DNA.
Kwa
muda mrefu polisi ya Uganda ilikuwa imetoa amri ya kutiwa mbaroni
kiongozi huyo wa waasi wa ADF mwenye umri wa miaka 51 kwa tuhuma za
kufanya mauaji ya kigaidi na kuiomba Interpol iisaidie kumkamata.
Mukulu
aliyekuwa muumin wa kanisa Katoliki kabla ya kuhamia Uislam, alianzisha
kundi hilo la ADF mnamo miaka ya 1990, kwa ajili ya kupingana na
serikali ya Uganda.
Tangu
hapo amekuwa akiongoza waasi katika mapigano ambayo yamepoteza maisha
ya maelfu ya raia wa Uganda na DRC. Mukulu anakabiliwa na makosa ya
ugaidi na uhaini.
Taarifa
ya Umoja wa Mataifa inasema mwaka 1998, waasi wa ADF walifanya mauaji
ya kinyama ya wanafunzi 80 walipokivamia chuo kimoja magharibi mwa
Uganda.
Mwezi Novemba mwaka jana waasi hao waliwaua watu zaidi ya 100 ikiwa ni mwendelezo wa mashambulizi ya kutisha Mashariki mwa DRC.
CHANZO: BBC SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni