Mwenyekiti
wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam jana, ambapo alipinga Msajili wa Vyama
Siasa Nchini, Jaji Francis Mtungi kubadilisha jina la chama cha
ACT-Tanzania na kuwa ACT-Wazalendo kwa anachodai bila ya kufuata
utaratibu.
Viongozi
wa chama hicho wakiwa meza kuu. Kutoka kushoto Kaimu Katibu wa chama
hicho, mkoa wa Dar es Salaam, Peter Katunka, Kaimu Katibu Mkuu, Leopold
Mahona, Mwenyekiti, Kadawi Lucas Limbu na Katibu Muenezi Fredy Kisena.
Mwenyekiti wa ACT-Tanzania, Lucas Kadawi Limbu akionesha kadi.
MWENYEKITI
wa Chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Tanzania), Lucas
Kadawi Limbu amemlalamkia Msaji wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Mstaafu
Francis Mtungi kwa madai ya kukiuka utaratibu wa kubadilisha jina la
chama hicho na kuwa ACT-Wazalendo.
Limbu alitoa malalamiko hayo mbele za waandishi wa habari Dar es Salaam jana na kuhoji nyuma ya ACT-Wazalendo kuna nini.
"Tunashangazwa
na jaji Mtungi kwa kubadili jina la chama chetu bila ya kufuata
taratibu huku akijua fika kuna kesi ya msingi ipo mahakama kuhusu
mwenendo wa chama hicho",alisema Limbu.
Aliongeza
kuwa kuna njama za makusudi zilizofanywa za kubadilisha jina la chama
hicho kwani haiwezeka na haiingii akilini kubadilisha jina la chama kwa
kipindi kifupi na haraka kiasi hicho.
"ACT-Tanzania
ni chama chetu sio cha Zitto na kama anahitahi siasa safi aanzishe
chama chake kwani nafasi hiyo ipo wazi kwa kila mtanzania.
Alisema
ni jambo la ajabu kuona chama kinafanya mkutano wake mkuu wenye nia hofu
na kumpatia mtu madaraka ya kioongozi mkuu na kubadilisha jina lake
huku msajili wa vyama akishuhudia.
Alisema
msajili wa vyama vya siasa alitoa tamko la kubadilishwa jina la chama
hicho tarehe 20-4-2015 wakati tayari kiongozi mkuu wa chama hicho
kilichobadilishwa jina akiwa katika zaira ya kichama mikoani aliyoianza
tarehe 10-4-2015 huku wakigawa kadi kwa kupitia chama cha ATC-Wazalendo.
Limbu
alihoji fedha zinazotumika kwenye ziara hiyo na za kuchapa kadi, bendera
za chama na vifaa vingine kuwa zinatoka wapi kama hakuna watu wenye nia
mbaya na chama cha AUT-Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni