Wakimbizi saba Raia wa Burundi wamepoteza maisha katika kipindi cha wiki moja kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Kuhara eneo la Kagunga mjini Kigoma magharibi mwa Tanzania.
Shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR linashirikiana kwa karibu na serikali ya Tanzania kuzuia kuenea kwa ugonjwa wa kuhara katika Kambi. Maelfu ya raia wa Burundi wanaotoroka mzozo wa kisiasa nchini mwao wanaingia nchini Tanzania kupitia mji wa Kigoma katika kijiji cha Kagunga kwa ajili ya kupatiwa hifadhi.
Dr.Patson Njogu afisa kutoka shirika la kuhudumia wakimbizi na hapa anaeleza mazingira ya tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni