ZIKIWA
zimebaki siku nne, kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya wavulana ya
Iyunga, kurejea shuleni kuendelea na masomo baada ya kufungwa kwa wiki
tatu kufuatia ajali ya moto ulioteketeza mabweni na mali za wanafunzi
151, bado hali imeonekana kuwa tete baada ya baraza la madiwani la
Halmashauri ya Jiji la Mbeya, kuendelea kugoma kupitisha maombi ya
shilingi milioni 235.
Madiwani
hao, wamekuwa wakihoji uhalali wa kiasi hicho cha fedha, kilichoombwa
na halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya kuanza kwa ukarabati wa
mabweni, utengenezaji wa vitanda na ununuzi wa vifaa mbalimbali kwa
wanafunzi 151, ikiwa baadhi ya wadau mbalimbali wamewasilisha michango
yao ambayo thamani yake haijahainishwa na wala taarifa ya mapato na
matumizi haijawasilishwa kwa kamati husika .
Mbali
na hilo, pia kamati ya fedha ilipoketi mapema mwezi huu, ilishindwa
kufikia muafaka wa kupitisha matumizi hayo ya fedha na kuwataka
wataalamu wa idara husika kuhakikisha wanaainisha vitu vyote
vilivyopokelewa kama msaada ikiwa na kufahamu thamani yake, ili kufahamu
ni kiasi gani halali kinachohitajika kutolewa na halmashauri hiyo.
Pia,
wajumbe hao wamelalamika kutoshirikishwa kwenye mambo mengi yanayoihusu
dharura hiyo ya ukarabati wa shule ya Iyunga, kufuatia ajali hiyo ya
moto huku wakitolea mfano, harambee ya kwanza iliyodaiwa kuitishwa na
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Munasa Nyirembe kwa madai kuwa ilikuwa si
halali kwani mpaka sasa taarifa zake za fedha zimekuwa zikighubikwa na
utata.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni