Umoja wa Afrika umeendelea kutiwa wasiwasi na hali ya kisiasa na
usalama nchini Burundi, baada ya mazungumzo ya kisiasa kusimama ghafla,
huku mpatanishi wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Burundi, Said
Djinnit akijiuzulu kufuatia ombi la vyama vikuu 17 vya upinzani na
mashirika ya kiraia yanayopinga muhula wa tatu wa rais Pierre
Nkurunziza.
Katika mkutano wa kilele wa 25 wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Johannesburg Jumapi
li
Juni 14, Umoja huo umeamuaa " kupelekwa haraka timu ya waangalizi wa
Haki za Binadamu na wataalamu wa kijeshi kutoka Umoja wa Afrika na Umoja
wa Ulaya watakaosimamia mchakato wa kuwapokonya silaha wanamgambo
pamoja na makundi mengine yenye silaha nchini Burundi ", Smail Chergui,
Kamishna wa Amani na Usalama, ametangaza Jumatatu Juni 15.
Hayo
yanajiri wakati ujumbe wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki umewasili
tangu Jumapili usiku mjini Bujumbura. Ujumbe huo unaoundwa na mawaziri
wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana Jumatatu wiki
hii na rais Pierre Nkurunziza na vyama vikuu vya upinzani.
Mpaka
sasa serikali ya Burundi bado inashikilia msimamo wake wa kufanyika kwa
uchaguzi mkuu kulingana na kalenda mpya ya uchaguzi iliyotangazwa hivi
karibuni
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni