Sudan Kusini imeupinga wito wa Umoja wa Mataifa wa kuitaka ibatilishe
uamuzi wake wa kumtimua mjumbe mkuu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa
Mataifa nchini humo. Nchi hio ilisema Toby Lanzer mratibu mkuu wa
misaada ya kiutu wa Umoja huo, aliikosoa serikali mara kwa mara na kuwa
alivuka mipaka kwa kusema serikali ya nchi hiyo inaelekea kuanguka
Msemaji Mkuu wa rais wa Sudan Kusini Ateny Wek Ateny, amezungumza kuwa
ni vigumu kubadilisha uwamuzi wa kumfukuza nchi Toby Lanzer. Na kuongeza
kuwa baraza la mawaziri lilitoa uwamuzi huo, baada ya kutathmini maoni
ya mara kwa mara ya mjumbe huyo dhidi ya serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni