Hatua ya Robo Fainali ya michuano
ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa
kuendelea kesho Jumatano kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam, huku macho na masikio yakiwa kwenye mchezo
kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC.
Mechi hiyo ya pili inatarajiwa
kuanza saa 10:15 jioni inatarajiwa kuwa ya vuta nikuvute kufuatia timu
hizo mbili zinatotokea jijini Dar es salaam kuwa na upinzani mkali
kuanzia katika Ligi Kuu a Vodacom Tanzania na michuano mingine.
Kocha mkuu wa Azam FC, Stewart
Hall amesema hana cha kuogopa katika mchezo huo dhidi ya Yanga, vijana
wake amewandaa kupambana katika hatua hiyo ya robo fainali na ana imani
wataibuka na ushindi.
Stewart ameongeza kuwa ana wigo
mpana wa kikosi chake, katika hatua ya makundi wameweza kushinda michezo
yao yote mitatu na kufunga mabao 8, huku ukuta wake ukiwa haujaruhusu
bao hata moja kuingia wavuni kwake.
Kwa upande wa Yanga, kocha Hans
Van der Pluijm amesema naaiheshimu klabu ya Azam, na katika mchezo wa
kesho hana cha kupoteza, kikosi chake kimemalilika kila idara kuelekea
katika hatua ya robo fainali.
Hans anajivunia kikosi chake
ambacho kimeonyesha mabadiliko makubwa kutoka mchezo wake wa awali
iliyoupoteza, na kushinda michezo mitatu mfululizo iliyofuatia katika
hatua ya makundi.
Mchezo wa kwanza wa robo fainali
utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy ya Sudan, mechi
itakayoanza saa 7:45 mchana uwnaja wa Taifa jijini Dar es aalaam.
Wakati huo huo Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NMB nchini Tanzania Ineke Bussemaker anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa robo fainali kesho kati ya Azam FC
dhidi ya Yanga SC.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni