Wakizungumza kwa uchungu waathirika hao wamelalamikia kuendelea
kuishi maisha magumu kutokana na uchakavu wa mahema ambapo baadhi yao
wanalala nje na watoto na kuishi kwa kutegemea viazi vitamu kusukuma
maisha ambapo wameomba serikali kuona huruma kwa watu hao kutokana na
maisha magumu wanayoishi.
Nae mtafiti kutoka taasisi ya naliendele Bernadeta Kimata
akizungumza na wananchi hao amesema waliliona hilo na ndio maana
wakagawa mbegu za viazi bure kwa wananchi ili kuwezesha waathirika hao
kupata chakula kwa muda mfupi kuwawezesha kukabiliana tatizo la njaa
ambapo wamewataka walime viazi kwa wingi viwasaidie kupunguza ugumu wa
maisha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni